Jumanne, Oktoba 25, 2016
Jumanne, Oktoba 25, 2016,
Juma la 30 la Mwaka wa Kanisa
Ef 5: 21-33;
Zab 128: 1-5;
Lk 13: 18-21
UFALME WA MUNGU-UPO NA BADO UTAKAMILIKA
Katika somo la kwanza Mtume Paulo anaendelea na maelekezo yake kwa Waefeso jinsi ya kuenenda kama wafuasi wa Kristo na leo anaingia katika ngazi ya familia. Anawaambia wake wawatii waume zao na waume wawapende wake zao. Ni katika kuendeleza tunu hizi katika familia ndipo twaweza kusema kuwa tunajenga ufalme wa Mungu katika familia zetu. Tunapoishi vizuri na wenzetu kwa upendo na kwa fadhili za Kimungu kama alivyotufundisha Kristo tunakuwa tunaishi Ufalme wa Mungu tungali hapa duniani. Ni katika kuuishi vizuri ufalme huo hapa duniani inatupa kibali cha utimilifu wake katika maisha yajayo. Yesu anatoa mifano miwili katika akilielezea Ufalme huu wa Mungu.
Ni ufalme ghani unao hubiriwa na Yesu? Mfano wa punji ya haradali na chachu unaelezea sifa za muhimu za Ufalme wa Mungu alio hubiri Yesu: udogo wake, tabia yake yakutokuonekana kirahisi; kazi yake na uwepo wake.
Yesu leo anafananisha ufalme wa Mungu na punji ya haradali na chachu. Puche ya haradali ni ndogo tena sana. Inapopandwa ardhini inakuwa na kuwa mti mkubwa ambapo ndege wa angani hupata makao. Lakini, pamoja na kwamba ni ndogo, na haijulikani na kujificha inapokuwa ardhini haibaki hapo tu bali huchipua na kumea. Chachu kidogo sana, ambayo huwezi kuiona kwa macho baada ya kuwekwa katika unga, haibaki kama ilivyo bali huumua unga wote.
Tabia ya Uwepo wake na utimilifu wake ujao wa Ufalme wa Mungu unaweza kuwa wetu tu kama matunda ya kazi ya Roho Mtakatifu.
Sala: Bwana, tunaomba ufungue macho yetu tuweze kutambua maajabu ya Ufalme wako, uliojificha na uwepo wake katika mambo madogo. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni