Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Agosti 12, 2019

Jumatatu, Agosti 12 2019
Juma la 19 la Mwaka

Kum 10:12-22;
Zab 147:12-15, 19-20;
Mt 17:22-27

TUMECHAGULIWA KWA LENGO!

Mamilioni ya watu wanajiuliza maswali. “Kwanini mimi nipo hapa?” na “ni nini maana ya mimi kuwepo?”. Haya maswali yamekuwa kama somo katika falsafa, sayansi, na katika elimu ya Mungu siku zote katika historia. Eleanor Roosevelt anasema “lengo la maisha ni kuyaishi, kuyaonja, na kuyazoea katika hali ya juu, na kutoka nnjee kwa ujasiri bila woga wa kupata mambo mapya na utajiri wake”. Na Ralph Waldo Emerson anaiweka hivi “ lengo la maisha sio kuwa na furaha. Nikuwa mwenye faida (kutumika), kuheshimiwa, kuwa na huruma, na kuifanya ifanye mabadiliko kwa yale ulioshi na kuishi vizuri”.

Katika Injili ya leo, kwa mara ya pili, Yesu anajulisha lengo lake la kuja ulimwenguni kwa kuongelea kuhusu mateso kifo na ufufuko kwa wafuasi wake. Anaeleza kwamba lengo lake kuja ulimwenguni sio kuja ili wamfanye mfalme wa kidunia, bali kuokoa ulimwengu kutoka dhambini nakudhihirisha thamani ya ufalme wa mbinguni. Kwa kuwa Mkristo pia nimeitwa kutambua lengo la maisha ni kuwa raia mwaminifu wa duniani na mbinguni. Ni nini jukumu langu? Je, natambua lengo la maisha yangu? Bado unakumbuka mafundisho ya Katekisimu ya kanisa Katoliki ya kwanini Mungu ametuumba?

Sala:
Bwana, nisaidiye mimi nitambue lengo la maisha yangu niweze kuwa raia mwema katika dunia, nchi yangu na zaidi sana wa mbinguni.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni