Jumatano, Agosti 07, 2019
Jumatano, Agosti 7 2019
Juma la 18 la Mwaka
Hes 13: 1-2, 25 – 14: 1, 26-29, 34-35;
Zab 95: 1-2, 6-9 (K) 8;
Mt 15: 21-28.
WOTE WATOTO WA MUNGU
Tukio la Yesu kukutana na mwanamke Mkananayo inadhihirisha kuwa, Watu wa Mataifa hawatajitenga na Taifa la Israeli. Mwanamke huyu Mkananayo ni fundisho kubwa juu ya Imani, na ni miongoni wa ukoo wa Wakaanani wa mwanzo waliokuwa adui wakubwa wa Kibiblia wa Taifa la Israeli, ambao upagani wao ulipelekea kwa Taifa la Israeli kutenda dhambi ya kuabudu miungu wengine.
Jibu alilotoa Yesu kwa yule mwanamke halimaanishi kuwa alimshtaki bali alijaribu kumpima apate kuona imani yake kwake. Lakini Yesu hamaptii jibu la ombi lake papo kwa papo, bali anajaribu kumfanya mwanamke huyo apate kumtambua Yeye ni nani, na pia atambue kazi iliyomleta hapa duniani, Pia Yesu anataka kumpa fundisho huyu mwanamke kuwa Yeye amekuja kwanza kwa ajili kondoo waliopotea wa Israeli.
Mwanamke huyo anatambua kuwa Yesu ni mwana wa Daudi, kwa kusema hivyo tayari anakuwa amemkubali Yesu kama mfalme wa taifa ambalo liliwashinda baba zao hapo kale. Pia tukumbuke kuwa mwanamke huyu hakukataa kuwa Yesu amekuja kwaajili ya waisraeli, anachoamini ni kwamba Yesu anao uwezo pia wa kuwahudumia watu wa mataifa mengine. Hoja hiyo inamgusa sana Yesu, kwani alikuwa amewalisha wana wa Israeli mkate na samaki na yakabaki makapu kumi na mawili ya mabaki. katika maelezo haya, mwinjili Mathayo anataka kuwakumbusha waisraeli kuwa, watu wa mataifa na wana wa Israeli wenyewe wanaweza kumfikia Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo kama mwokozi wao.
Sala:
Bwana wafanye watu wote waonje upendo wako kwao kwa kupitia kwangu.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni