Ijumaa, Agosti 02, 2019
Ijumaa, Agosti 2, 2019
Juma la 17 la Mwaka
Wal. 23:1,4-11,15-16,27,34-37
Zab 8:2-5, 9-10 (k) 1,
Mt. 13:54-54
UDONGO WENYE RUTUBA WENYE KUPOKEA BARAKA ZA MUNGU
Yesu alitembelea katika mji wake mwenyewe Nazareth lakini anashangaa watu hawapo tayari kumkaribisha na kupokea ujumbe wa habari njema. Hawakatai tu kumwamini na ujumbe wake na miujiza yake, wanamhukumu kwa kutazama historia ya maisha yake ya kifamilia. “huyu si mwana wa seremala?” Mama yake sio Mariam? Walimtazama yeye kama mtu wa kawaida tu. Na hivyo wanazuia ufalme wa Mungu unaokuja katikati yao.
Sehemu hii inatufundisha sisi kwamba tuwe tayari kuwasikiliza wenzetu, hasa wale waliojifunza na wenye hekima hata kama ni ndugu zetu. Kwani Mungu anaweza kutufundisha sisi hata kwa kutumia ndugu zetu wa familia. Pili tunapaswa kujirekebisha hasa tunapo amua kumhukumu mtu kwa kutumia familia yake au historia yake. Watu wote hawabaki walivyo kama zamani. Tunapaswa kuwatazama watu katika hali ya mtazamo mpya na sio kumfungia katika kisanduku kwamba hatabadilika. Tatu, mara nyingi tunasikia mandiko matakatifu kupitia kwa watu mbali mbali, tunapaswa kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu anaye ongea nasi kwa njia ya mtu huyo. Nne, usikatishwe tamaa na mtu aliyekuchukia kwasababu ya hali ya familia yako au ahali yako ya zamani, au kwasababu hakupendi. Zaidi ya yote usiache kutenda mema kwa watu wote.
Mabadiliko ya kweli kwa roho za watu wa Nazaret hazikubadilika kwasababu ya kukosa Imani. Watu hawakuwa tayari kupokea maneno ya Yesu yazame katika mioyo yao na akili zao. Kwa njia hiyo, Yesu, hakuweza kufanya miujiza mikuu huko katika mji wake wenyewe.
Je, unamruhusu Yesu abadilishe kila kitu katika maisha yako ya kila siku? Je, upo tayari kumfanya afanye miujiza mikubwa katika maisha yako? Kama una wasi wasi katika kujibu maswali haya ni dalili kwamba unamhitaji Mungu afanye mabadiliko katika maisha yako.
Sala:
Bwana, ninaomba roho yangu iweze kuwa udongo mzuri wa kuotesha neno lako. Ninaomba roho yangu iweze kubadilishwa nawe, paweze kuwa sehemu ya neno lako na uwepo wako. Ninaomba unibadilishe mimi na kunifanya niweze kuwa chombo cha Amani ya neema yako. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni