Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Julai 15, 2019

Jumatatu, Julai 15, 2019.
Juma la 15 la Mwaka wa Kanisa

Kut 1:8-144, 22;
Zab 124:1-8;
Mt 10:34 – 11:1.

UKWELI UTAKUWEKA HURU
Yesu aliwaambia mitume wake: “mnadhani nimekuja kuleta Amani duniani? Sikuja kuleta Amani bali upanga”. Huu ni moja ya useme ambao waweza kutuacha tukiwa tuna shangaa na kuchanganyikiwa. Je, ni kweli Yesu alitaka kuleta “upanga”? na utengano licha ya Amani?
Ukweli wa Injili una uwezo wa kutu unganisha na Mungu kama tutaipokea kama Neno la kweli. Lakini pia linatutenganisha na wale wanao kataa kuunganika na Mungu katika kweli. Tamaduni zetu siku hizi zinapenda kutangaza hali ya “umimi”. Hii ni hali ya kilicho kizuri kwangu na kweli kinaweza kisiwe kizuri kwako, na kwamba licha ya hayo ya kila mtu kuwa na ukweli wake, tunaweza kuwa na furaha kama familia yenye furaha. Lakini huo sio ukweli! Ukweli ni kwamba Mungu ameanzisha kilicho chema na kama sio chema ni kibaya. Ameweka sheria yake ya maadili katika ubinadamu wetu na hili haliwezi kukataliwa. Ameweka pia ukweli wa imani yetu na hilo hatuwezi kulikataa. Na sheria hiyo ni kweli kwako na kwangu pia, na kwa yeyote yule. Kwa kushikilia ukweli, tunaweza kutengana hata na wale ndugu zetu wa familia. Yesu anatupa maneno haya kutupa nguvu na kutuonesha kwamba haya yakitokea tusiogope. Yesu, alikataliwa na hivyo tusishangae kama hayo yakitokea kwetu pia.
Tafakari leo, ni kwa jinsi ghani ulivyo tayari kupokea ukweli wa Injili licha ya matokeo yake. Ukweli kamili utakuweka huru na utafunua ukweli kuhusu wale walio jitenga na Mungu.

Sala:
Bwana, ninakuomba unipe hekima na nguvu yakuweza kupokea yote ulio tufunulia. Nisaidie mimi nikupende wewe zaidi ya yote na kupokea matokeo yote yatokanayo na kukufuata wewe. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni