Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Mei 24, 2019

Ijumaa, Mei 23, 2019,
Juma la 5 la Pasaka

Mdo 15: 22-31;
Zab 57: 8-12 (K. 10);
Yn 15: 12-17.

TUMECHAGULIWA KUWA WA MUNGU!
Watoto wanapenda kucheza michezo. Wakati mchezo unaundwa kwa pande mbili, watoto wanaunga mstari wakisubiri kuchaguliwa. Kila mtoto anategemea kuchguliwa wa kwanza. Inaonesha hamu ya ndani ya kutaka kuchaguliwa kwa ajili ya mchezo. Hili linaonesha hamu iliyopo ndani ya kila mmoja wetu ya kuchaguliwa. Uzuri ni kwamba, Mungu anamchagua kila mmoja wetu. Anatutaka sisi kuwa watoto wa familia yake na anatutaka tuwe watu wake. Hili ni la muhimu kulielewa na likieleweka linadhihirika. Mungu alituchgua sisi hata kabla hatuja zaliwa. Anatufahamu kabla, tangu milele yote na anaweka jicho lake juu yetu, akilenga kutuleta sisi katika kundi lake. Tunapaswa kutambua hili, kulikubali na kuliamini. Sisi ni wake.

Mungu hatuchagui sisi tu kuwa wake, anatuchagua pia kwa utume. Anataka kututumia sisi tuzae matunda kwa Ufalme wake. Anataka kututumia sisi kwa malengo matakatifu na wito wa Kimungu. Haijalishi ni mara ngapi tunaweza kujiona “hatustahili” tunaweza kujisikia kufanya utofauti, tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu hatuoni katika hali hiyo. Bali, anaona utajiri mkubwa ndani ya kila mmoja wetu na kuchagua kutumia utajiri huo kujenga ufalme wake.

Mungu anakuambia “nimekuchagua wewe” na “Nenda ukazae matunda”. Kukubali wito wako kutoka kwa Mungu utabadilisha maisha yako na pia yatabadilisha maisha ya wale ulioitwa kuwatumikia.

Sala:
Bwana, ninatambua umenichagua mimi. Ninakubali wito wako katika maisha yangu. Ninakubali ukweli kwamba umenichagua mimi katika hali ya utume wa pekee na hali ya utukufu wa pekee. Nisaidie daima niendelee kusema “ndio” kwa wito wako. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni