Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Oktoba 17, 2016

Jumatatu, Oktoba 17, 2016,
Juma la 29 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Mt. Ignasio wa Antokia, Askofu na Mfiadini

Ef 2:1-10
Zab 100:2-5
Lk 12:13-21


KUWA TAJIRI KUMWELEKEA MUNGU!

Katika somo la kwanza, Mt. Paulo, kwa barua yake kwa Waefeso, inatoa ufafanuzi mzuri kuhusu kazi ya Mungu ya ukombozi ndani ya Yesu Kristo, kwa mapendo yake kwa wanadamu. “Mungu ambaye ni mwingi wa huruma” anasema, “kutoka katika mapendo yake makubwa aliotupenda nayo, hata tulipokufa katika dhambi kwa njia ya makosa yetu, alitufanya hai pamoja na Kristo”. Anamalizia na kitu ambacho Mungu anategemea katika maisha yetu: “sisi tupo kwa jinsi alivyo tuumba, alituumba katika Kristo kwa kazi njema alio andaa Mungu mbele yetu iwe njia yetu ya maisha”. Mfano uliopo katika Injili kuhusu tajiri mpumbavu unatoa mlio kamili wa tafakari ya somo la kwanza. Baada ya kuelezea nafasi ya tajiri bahili asiyetaka kumpa Mungu chochote kwa yale anayopata, na kudhani yote ni mali yake, kutumia anavyopenda, Yesu anasema wazi “ni kama wale wanaojiwekea akiba kwa ajili yao binafsi na wala sio matajiri katika kumwelekea Mungu”. Mungu kwa njia ya upendo ametupa sisi, sio tu vitu mbali mbali bali kitu muhimu kabisa, zawadi ya Imani yetu ndani ya Yesu Kristu iliotuletea ukombozi. Pia, “na kila mmoja aliyepewa vingi, vingi vitatakwa kwake, na kwa aliyekabidihiwa vingi, vingi vitatakwa zaidi”, (Lk 12:48).

Hatuwezi kusema tunakuwa ‘watu wema zaidi’ kwasababu ni wakarimu, “Mungu aliandaa haya kabla, yawe njia yetu ya maisha”. Kwahiyo, hatuwezi kusema tunanunua ukombozi wetu kwasababu tunafanya matendo mema. Mt. Paulo anaeleza wazi kwamba, “kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya Imani, na hili sio kwamba mmelisababisha ninyi, bali ni zawadi ya Mungu-sio matokeo ya kazi zenu”. Kwasababu tumepokea zawadi ya ukombozi, tunapaswa kuwa watu wa matendo ya huruma, na sio kinyumbe chake . Kwa hiyo, Yesu anatuambia kuwa “tuwe matajiri katika kumwelekea Mungu” ambaye amekuwa mkarimu bila kipimo juu yenu. Kwa maneno mengine, muwe wakarimu katika kufanya mapenzi yake, kwa kushika amri zake, kwa kumpa utukufu kwa kila kitu unachofanya.

Sala: Bwana, nakushukuru kwa zawadi zako. Nisaidie niweze kuwashirikisha wengine. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni