Ijumaa, Mei 17, 2019
Ijumaa, Mei 17, 2019,
Juma la 4 la Pasaka
Mdo 13: 26-33;
Zab 2: 6-11;
Yn 14: 1-6.
MBINGUNI NI NYUMBANI KWETU!
Mara kwa mara ni muhimu kuweka jitihada kuelekea kwenye utukufu wa Mbinguni! Mbingu ipo na ni mapenzi ya Mungu sisi wote siku moja tufurahi na Utatu Mungu mmoja. Kama tunatambua kwa hakika kuhusu mbingu, tunakuwa tunaitamani kwa moyo wote na tunawaka mapendo na kuitazamia kwa nguvu kubwa, tukiwa tumejazwa na Amani na furaha kila wakati tuki ifikirie. Kwa bahati mbaya, habari za kuacha ulimwengun huu na kwenda kukutana na Muumba wetu kwa wengi zina ogopesha. Pengine ni hofu ya mambo yasio julikana, utambuzi wa kwamba tutawaacha wapendwa wetu, au hofu ya kwamba huenda tusiende mbinguni.
Kama Wakristo, ni vizuri kujishughulisha tukitambua upendo wetu mkubwa mbinguni kwa kupata utambuzi mkubwa wa sio mbinguni pekee, bali kutambua jukumu la maisha yetu hapa duniani. Mbingu inasaidia sisi tuweze kupanga maisha yetu kwa kupitia ile njia inayo tuongoza kwenye heri hiyo. Katika Injili, tunapewa picha nzuri sana yenye kufariji kuhusu Mbinguni, ambayo ni “Nyumba ya Baba”. Nyumbani ni sehemu salama. Ni sehemu ambayo tunaweza kufurahia na kuishi bila kujifanya, kuwa na wapendwa wetu, kupumzika, na kujisikia ni sehemu ya familia. Sisi ni watoto wa Mungu na hivyo Mungu anapenda sisi tuwe nyumbani pamoja naye.
Kwa kutafakari juu ya picha hii, inapaswa pia iwe faraja kwa wale wote waliopoteza wapendwa wao. Hali ya kusema kwaheri, ni ngumu. Na inapaswa kuwa ngumu. Ugumu wa kupoteza wapendwa wetu inaonesha uwepo wa upendo wa kweli katika mahusiano. Lakini Mungu anapenda hali ya hisia za kupoteza wapendwa wetu ichanganyike na furaha tunapo tafakari ukweli wa wapendwa wetu kuwa wapo na Baba nyumbani milele. Wana furaha kule zaidi ya jinsi tunavyo weza kudhania, na siku moja nasi tutaitwa kushiriki furaha hiyo.
Sala:
Bwana, natamani daima kuwa nawe. Nisaidie daima niweke lengo hili daima akilini mwangu, na kukuwa nalo siku zote kwa tamaa ya kufurahi nawe milele. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni