Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Mei 16, 2019

Alhamisi, Mei 16, 2019.
Juma la 4 la Pasaka

Mdo 13:13-25;
Zab 89:2-3,21-22,42:225,27 (K. 2);
Yn 13:16-20.

TUME BAHATIKA KUWA “WATUMWA”
“Nawaambieni, hakuna Mtumwa aliye mkubwa kuliko Bwana wake, na wala hakuna mjumbe aliye mkuu kuliko yule aliye mtuma”. Yesu anajaribu kutuambia vitu viwili. Cha kwanza, ni vizuri kujiona sisi wenyewe kama watumwa na wajumbe wa Mungu na pili tunapaswa kumpa Mungu utukufu wote. Hili ni jambo muhimu la kuishi katika maisha ya kiroho.

Kawaida habari ya kuwa “mtumwa” haitamaniki sana. Na kilicho kibaya kuhusu utumwa ni kutendwa vibaya na Bwana wao. Wanatendwa vibaya na kuonekana kama vitu tu tofauti na utu wao wa kibinadamu. Lakini chukulia hali nyingine ambapo mmoja ni mtumwa alafu Bwana wake anampenda na jambo lake la kwanza kabisa la Bwana huyu ni kumsaidia huyu “mtumwa” ili atambue talanta zake ili aweze kukamilisha malengo yake ya maisha. Katika hali hii, “Bwana” huyu anamfanya mtumwa kuwa na upendo na furaha na wala hata haribu utu wake wa kibinadamu.

Hali hii ndivyo ilivyo kwa Mungu. Hatupaswi kukataa habari ya kuwa watumwa wa Mungu. Katika hali ya kweli, tunapaswa tutamani Mungu awe Bwana wetu zaidi kuliko hata tunavyo tamani kuwa mabwana sisi wenyewe. Kwani Mungu atatutenda vizuri zaidi kuliko hata sisi wenyewe. Kwani atatupa maisha ya utakatifu na furaha na kwa unyenyekevu kutuweka katika mapenzi yake. Atatupa vyote tunavyo hitaji kwa ajili ya kutenda yale anayo tuamuru. Kuwa “Mtumwa wa Mungu” ni kitu kizuri na tunapaswa kutamani mpango huo katika maisha.

Sala:
Bwana, ninajikabidhi katika kila unacho niamuru. Ninaomba mapenzi yako yakamilike kwangu, mapenzi yako tu. Ninakuchagua wewe kuwa Bwana wangu katika kila kitu na ninaamini upendo wako mkamilifu kwangu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni