Alhamisi. 03 Aprili. 2025

Sala

Sala ya Usiku

Sasa siku imekwisha,
Kwako Mungu napandisha,
moyo wangu kwa shukrani,
nipumzike kwa amani,

Mema mengi umenipa,
ninashindwa kukulipa,
Baba mwema ondolea,
yote niliyokosea.

Yesu mpenzi unijie,
ombi langu usikie,
unifiche mtoto wako,
ndani ya jeraha zako,

Ewe Mama unipe neema,
raha na usiku mwema,
Roho mlizi ukakeshe,
pepo wasinikoseshe

Naiweka roho yangu,
mikononi mwa Baba yangu,
bila hofu napumzika,
mwisho kwake nitafika.

Amina

Maoni


Ingia utoe maoni