MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
1. Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
2. Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
3. Yesu anazaliwa Bethlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
4. Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
5. Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
0 Imependwa
0 Maoni
Maoni
Ingia utoe maoni