Jumatano. 11 Septemba. 2024

Sala

Litania ya Bikira Maria

LITANIA YA BIKIRA MARIA

Bwana utuhurumie. Bwana utuhurumie.

Kristo utuhurumie.
Kristo utuhurumie.

Bwana utuhurumie. Bwana utuhurumie.

Kristo utusikie. Kristo utusikilize

Baba wa mbinguni, Mungu, utuhurumie.

Mwana Mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie.

Roho Mtakatifu, Mungu, utuhurumie.

Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja, utuhurumie.

Kiitikio: Utuombee
Maria Mtakatifu,
Mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Bikira Mtakatifu, Mkuu wa mabikira,
Mama wa Kristu,
Mama wa neema ya Mungu,
Mama mtakatifu sana,
Mama mwenye usafi wa moyo,
Mama usiye na doa,
Mama usiye na dhambi,
Mama mpendelevu,
Mama mstaajabivu,
Mama wa shauri jema,
Mama wa Mwumba,
Mama wa Mkombozi,
Bikira mwenye utaratibu,
Bikira mwenye heshima,
Bikira mwenye sifa,
Bikira mwenye enzi,
Bikira mwenye huruma,
Bikira amini,
Kikao cha haki,
Kikao cha hekima,
Sababu ya furaha yetu,
Chombo cha neema,
Chombo cha heshima,
Chombo bora cha ibada,
Waridi lenye fumbo,
Mnara wa Daudi,
Mnara wa pembe,
Nyumba ya dhahabu,
Sanduku la Agano,
Mlango wa mbingu,
Nyota ya asubuhi,
Afya ya wagonjwa,
Makimbilio ya wakosefu,
Mfariji wa wenye uchungu,
Msaada wa Wakristu,
Malkia wa Malaika,
Malkia wa Mababu,
Malkia wa Manabii,
Malkia wa Mitume,
Malkia wa Mashaidi,
Malkia wa Waungama,
Malkia wa Mabikira,
Malkia wa Watakatifu wote,
Malkia uliyeumbwa, pasipo dhambi ya asili,
Malkia uliyepalizwa mbinguni,
Malkia wa Rozari takatifu,
Malkia wa amani.
****

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusamehe, Bwana.


Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusikilize, Bwana.


Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utuhurumie.

K. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristu.

TUOMBE: Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na ya mwili sikuzote. Tuopolewe na mashaka ya sasa kwa maombezi ya Maria mtakatifu, Bikira daima, ili tupate na furaha ya milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.

Maoni

Adamu Paul

Naomba mnitumie mwongozo wote wa rozali na kutania ya bikira Maria kwa njia ya sms hili niwe nasali hata njiani na mahali popote namba ni 0786191650

Leon Galabawa

Naomba mnitumie muongozo wote wa Rozali niweze kupandisha Imani yangu 0716664715

Wicliffe Okoth

naombea amani na uvumilivu katika nyumba yangu 0791071911

Frank Anthony

Naomba mwongozo wa kusali rozari takatifu na litania kwa njia ya Whatsapp 0786300892

Robert Muturi

Nashukuruni Sana nasikia Sasa nimesikika maombi yangu

LILIAN CHALE

TUMSIFU YESU KRISTU. NAOMBA UTUONGEZEE SALA YA MEMORARE, UIANDIKE IWE BAADA YA KUMALIZA LITANIA YA MAMA BIKIRA MARIA NA TUOMBE: Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na ya mwili sikuzote. Tuopolewe na mashaka ya sasa kwa maombezi ya Maria mtakatifu, Bikira daima, ili tupate na furaha ya milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina. MEMORARE UIONGEZEE KUANDIKA BAADA YA HII SALA. NATANGULIZA SHUKURANI ZANGU KWAKO. ASANTE.

Alexander Mbonde

Tumsifu YESU KRISTO naomba nitumieni sala yalozali.

PETERKENNEDY OPIYO

Naomba mnitumie mwongozo wote wa rozali na kutania ya Bikira Maria kwa kupitia Whatsapp ili niwe nasali hata nikitembea njiani na mahali popote. Namba ni 0769300937

Ingia utoe maoni