Masomo ya Misa
Sikukuu ya Bwana Wetu Yesu Kristo Kuhani Mkuu Mile (Alhamisi, Mei 24, 2018)
Yer. 31: 31 - 34
Angalia zinakuja siku, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya yuda. Si kwa mfano wa agano lilenililofanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana: Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika. Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema: Mjue Bwana, kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maananitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
Zab. 109:1a-e, 2,3
Neno la Bwana kwa Bwana wangu,
Uketi mkono wangu wa kuume,
hata niwafanyapo adui zako
kuwa chini ya miguu yako.
(K) Ndiwe Kuhani hata milele kwa mfano wa Melkisedeki.
Bwana atainyosha toka Sayuni
fimbo ya nguvu zako,
Uwe na enzi juu ya adui zako!
(K) Ndiwe Kuhani hata milele kwa mfano wa Melkisedeki.
Watu wako watajitoa kwa hiari,
siku ya uwezo wako;
kwa uzuri wa utakatifu,
tokea tumbo la asubuhi,
unao umande wa ujana wako
(K) Ndiwe Kuhani hata milele kwa mfano wa Melkisedeki.
Ebr 10: 11 -18
Kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zilezile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Na Roho Mtakatifu naye atushuhudia. Kwa maana, baada ya kusema: “Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana: Nitatia sheria zangu mioyoni mwao; na katika nia zao nitaziandika; Ndipo anenapo, Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.
Ebr 5:8 9
Aleluya, Aleluya,
Ingawa ni Mwana alijifunza kutii, kwa mateso yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.
Aleluya.
Mk 14: 22-25
Siku ya kwanza ya Mikate isiyochachwa, walipokuwa wakichinja Pasaka: nao walipokuwa wakila, alitwaa, mkate, akabariki, akaumega, akawapa, akisema: Twaeni; huu ndio mwili wangu. Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote. Akawaambia: Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. Amin, nawaambia ninyi: sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya katika ufalme wa Mungu.
Maoni
Ingia utoe maoni