Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Dominika ya 2 ya Majilio (Jumapili, Desemba 10, 2017)  

Somo la 1

Isa. 40:1-5, 9-11

Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umechiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dahmbi zake zote.

Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu, Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.

Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, panda juu yam lima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu.

Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, tahawabu yake I pamoja naye, na ijara yake I mbele zake. 

Atalilisha kundi lake kama mchungaji, atawakusanya wanakondoo mikononi mwake; na kuwachukua kifuani mwake, nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Wimbo wa Katikati

Zab. 85:8-13

Na nisikie atakavyosema Mungu Bwana, 

Maana atawaambia watu wake amani,

Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,

Utukufu ukae katika nchi yetu. 

(K) Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, utupe wokovu wako.


Fadhili na kweli zimekutana,

Haki na amni zimebusiana.

Kweli imechipuka katika nchi,

Haki imechungulia kutoka mbinguni. 

(K) Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, utupe wokovu wako.


Naam, Bwana atatoa kilicho chema,

Na nchi yetu itatoa mazao yake.

Haki itakwenda mbele zake,

Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia. 

(K) Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, utupe wokovu wako.

Somo la 2

2Pet. 3:8-14

Wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia,  bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba. Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo makuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. Kwa hiyo, wapenzi kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidi ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.

Shangilio

Lk. 3:4, 6

Aleluya, aleluya,

Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake. Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.

Aleluya.

Injili

Mk. 1:1-8

Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwitu. Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu. 

Maoni


Ingia utoe maoni