Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

KUMBUKUMBU YA MT. AMBROSI (Alhamisi, Desemba 07, 2017)  

Somo la 1

Isa. 26:1-6

Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; ataamuru wokovu kuwa kuta na mamboma. Wekeni wazi malango yake, taifa lenye haki, lishikalo kweli, uingie. Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika Amani kamilifu, kwa kuwa tunakutumaini.

Mtumainini Bwana sikuzote, maana Bwana Yehova ni mwamba wa milele. Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, mji ule ulioinuka, aushusha, aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini. Mungu utaukanyaga chini, naam, miguu yao walio maskini, na hatua zao walio wahitaji.

Wimbo wa Katikati

Zab. 118:1,8-9,19-21,25-27a

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema

Kwa maana fadhili zak eni za milele,

Ni heri kumkimbilia Bwana,

Kuliko kuwatumainia wanadamu,

Ni heri kumkimbilia Bwana

Kuliko kuwatumainia wakuu. 

(K) Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.


Nifungulieni malango ya haki,

Nitaingia na kumshukuru Bwana. 

Lango hili ni la Bwana,

Wenye haki ndio watakaoliingia.

Nitakushukuru kwa maana umenijibu,

Nawe umekuwa wokovu wangu. 

(K) Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.


Ee Bwana, utuokoe, twakusihi,

Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana,

Tumewabarikia toka nyumbani mwa Bwana.

Bwana ndiye aliye Mungu,

Naye ndiye aliyetupa nuru. 

(K) Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.

Shangilio

Isa. 55:6

Aleluya, aleluya,

Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni maadamu yu karibu.

Aleluya.        

Injili

Mt. 7:21,24-27

Siku ili, Yesu akawaambia wafuasi wake: Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba, mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Maoni


Ingia utoe maoni