Masomo ya Misa
Jumatano ya 24 ya Mwaka (Jumatano, Septemba 20, 2017)
1Tim. 3:14-16
Nakuandikia hayo, nikitaraji kuja huko hivi karibu. Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapatavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu:
Mungu alidhihilishwa
Katika mwili, akajulika
kuwa na haki katika
roho, akaonekana na
malaika, akahubiriwa
katika mataifa,
akaaminiwa katika
ulimwengu,
akachukuliwa juu
katika utukufu.
Zab. 111: 1-6
Haleluya.
Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote, barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
(K) Matendo ya Bwana ni makuu.
Matendo ya Bwana ni makuu, yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.
(K) Matendo ya Bwana ni makuu.
Kazi yake ni heshima na adhama, na haki yake yakaa milele.
(K) Matendo ya Bwana ni makuu.
Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; Bwana ni mwenye fadhili na rehema.
(K) Matendo ya Bwana ni makuu.
Amewapa wamchao chakula, atalikumbuka agano lake milele.
(K) Matendo ya Bwana ni makuu.
Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, kwa kuwapa urithi wa mataifa.
(K) Matendo ya Bwana ni makuu.
Lk 6: 63,68
Aleluya, aleluya,
Maneno yako, Bwana, ni roho na uzima.
Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Aleluya.
Lk 7:31-35
Bwana akasema, ''Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki, nao wamefanana na nini? Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, 'Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.' Kwa kuwa Yohane mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, ninyi mwasema, 'Ana pepo.' Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, nanyi mwasema, 'Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye zambi.' Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote."
Maoni
Ingia utoe maoni