Jumanne. 14 Mei. 2024

Masomo ya Misa

Jumamosi ya 23 ya Mwaka (Jumamosi, Septemba 16, 2017)  

Somo la 1

1Tim. 1:15-17

Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi. Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika katika mimi. Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristu audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele. Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu, Mungu peke yake, na iwe heshima na utufufu milele na milele.

Wimbo wa Katikati

Zab. 113:1-7

Aleluya.
Enyi watumishi wa Bwana, sifuni,
Lisifuni jina la Bwana,
Jina la Bwana lihimidiwe
Tangu leo na hata milele.
(K) Jina la Bwana lihimidiwe tangu leo na hata milele.

Toka maawio ya jua hata machweo yake
Jina la Bwana husifiwa.
Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
(K) Jina la Bwana lihimidiwe tangu leo na hata milele.

Ni nani aliye mfano wa Bwana,
Mungu wetu aketiye juu;
Anyenyekeaye kutazama,
Mbinguni na duniani?
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
(K) Jina la Bwana lihimidiwe tangu leo na hata milele.

Shangilio

Lk. 8:15

Aleluya, aleluya,
Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao, hulisikia neno la Mungu na kulishika.
Aleluya.

Injili

Lk. 6:43 – 49

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake. Na kwa nini mnaniita, Bwana, walakini hamtendi nisemayo? Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba yakawa makubwa.

Maoni


Ingia utoe maoni