Jumatano. 08 Mei. 2024

Masomo ya Misa

Kumbukumbu ya Kukatwa kichwa kwa Yohane Mbatizaji (Jumanne, Agosti 29, 2017)  

Somo la 1

1 Thes 2: 1-8;

Ninyi wenyewe, ndugu, mwakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure; lakini tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filipi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana. Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila; bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu. Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi. Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine tulipokuwa tukiweza kuwalemea kama mitume wa Kristo; bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe. Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.

Wimbo wa Katikati

Zab 138: 1-3, 4-6;

Ee Bwana umenichunguza na kunijua.
Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
(K) Ee Bwana umenichunguza na kunijua.

Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote.
Maana hamna neno ulimini mwangu
Usilolijua kabisa, Bwana.
(K) Ee Bwana umenichunguza na kunijua.

Umenizingira nyuma na mbcle,
Ukaniweka mkono wako.
Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi,
Hayadirikiki. siwezi kuyafikia.
(K) Ee Bwana umenichunguza na kunijua.

Shangilio

Mt. 4: 4

Aleluya, aleluya,
Mtu hataishi kwa mkate tu,
ila kwa kila neno litokalo
katika kinywa cha Mungu.
Aleluya.

Injili

Mk 6:17-29

Mfalme Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohane, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo ndugu yake; kwa kuwa amemwoa; kwa sababu Yohane alimwambia Herode, Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo. Nayeyule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate. Maana Herode alimwogopa Yohane; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha. Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya; ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa. Akamwapia, Lolote utakaloniomba nitakupa, hata nusu ya ufalrne wangu. Basi akatoka, akamwuliza mamaye, Niombe nini? Naye akasema, Kichwa cha Yohane Mbatizaji. Mara akaingia kwa haraka rnbele ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohane Mbatizaji. Mfalme akafanya huzuni sana, lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia. Mara mfalme akatuma askari, akaamuru kuleta kichwa chake. Basi, akaenda, akamkata kichwa mie gerezani, akakileta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, nayeyule kijana akampa mamaye. Wanafunzi wakewaliposikia habari, walikwenda, wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.

Maoni


Ingia utoe maoni