Masomo ya Misa
Jumatani ya 19 ya Mwaka (Jumatano, Agosti 16, 2017)
Kum 34: 1-12
Musa alipanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo, hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. Bwana akamwonyesha nchi yote ya Galiadi hata Dani; na Naftali yote, na nchi ya Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda, mpaka bahari ya magharibi; na Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari. Bwana akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko. Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la Bwana. Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo. Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazipunguka. Wana wa Israeli wakamwomboleza Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha. Na Yoshua. mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama Bwana alivyowamuru Musa. Musa, hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso; katika ishara zote na maajabu yote, ambayo Bwana alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote; na katika ule mkono wa nguvu wote, katika ule utisho mkuu wote, alioutenda Musa machoni pa Israeli wote.
Zab. 66 :1-3, 5, 8, 16-17
Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
imbeni utukufu wa jina lake,
tukuzeni sifa zake.
Mwambieni Mungu: Matendo yako yatisha kama nini.
(K) Ahimidiwe Mungu, aliyeweka nafsi yetu katika uhai.
Njani yatazameni matendo ya Mungu,
Hutisha kwa mambo awetendayo wanadamu.
Enyi mataifa, mtukuzeni Munug wetu,
itangazeni sauti ya sifa zake.
(K) Ahimidiwe Mungu, aliyeweka nafsi yetu katika uhai.
Njoni sikieni, ninyi nyotc mnaomcha Mungu,
nami nitayatangaza alivyonitendea roho yangu.
Nalimwita kwa kinywa changu,
na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu.
(K) Ahimidiwe Mungu, aliyeweka nafsi yetu katika uhai.
2 Kor 5: 19
Aleluya, aleluya,
Mungu alikuwa ndani ya Kristu,
akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.
ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Aleluya.
Mt. 18: 15-20
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Ndugu yake akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu: akikusikia, umepata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja an wawili. ili kwa vinywa vya mashahidi wawili a: watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia. na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote wata kaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu alive mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
Maoni
Ingia utoe maoni