Alhamisi. 09 Mei. 2024

Masomo ya Misa

Kumbukumbu ya Mtakatifu Maksimiliano Maria Kolbe (Jumatatu, Agosti 14, 2017)  

Somo la 1

Kum 10: 12-22

Sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; kuzishika amri za Bwana na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri? Tazama, mbingu ni mali za Bwana, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vili- vyomo. Tena, Bwana aliwafurahia baba zako, na kuwapenda, akawachagua wazao wao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo. Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu. Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiye- pendelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa. Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenye- we mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. Mche Bwana, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake. Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako. Baba zako walishukia Misri na watu sabini; na sasa Bwana, Mungu wako, amekufanya kama nyota za mbinguni kwa wingi.

Wimbo wa Katikati

Zab. 147:12-15,19-20

Msifu Bwana, ee Yerusalemu,
msifu Mungu wako, ec Sayuni.
Maana ameyakaza mapingo ya malango yako,
amewabariki wanao ndani yako.
(K) Msifu Bwana, ee Yerusalemu, au: Aleluya

Ndiye afanyaye amani mipakani mwako,
akushibishaye kwa unono wa ngano.
Huipeleka amri yake juu ya nchi,
neno lake lapiga mbio sana.
(K) Msifu Bwana, ee Yerusalemu, au: Aleluya

Humhubiri Yakobo neno lake,
na Israeli amri zake na hukumu zake
Hakulitenda taifa lo lote mambo kama hayo,
wala hukumu zake hawakuzijua.
Aleluya.
(K) Msifu Bwana, ee Yerusalemu, au: Aleluya

Shangilio

Yn 14: 5

Aleluya, aleluya,
Bwana anasema, mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima
Aleluya.

Injili

Mt. 17: 22-27

Mitume walipokuwa wakikaa Galilaya, Yesu akawaambia, Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua, na siku ya tatu atafufuka. Wakasikitika sana. Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa. Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa duniahutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? kwa wana wao au kwa wageni? Nave aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru. Lakini tusije tukawakwaza, ene- nda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli; ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.

Maoni


Ingia utoe maoni