Masomo ya Misa
Kumbukumbu ya Bikira Maria (Jumamosi, Agosti 12, 2017)
Kum. 6: 4-13
Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu. Bwana ndiye mmoja. Nawe inpende Bwana, Mungu wako. kwa moyo wako wote, na kwa roho yako vote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani. na ulalapo, na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako. Tena itakuwa atakapokwisha Bwana, Mungu wako, kukuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Ibrahimu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe, na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vimefukuliwa usivyofukua wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba; ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana alivekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa. Mche Bwana, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.
Zab. 18 :1-2, 46, 50
Wewe, Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana;
Bwana ni jabali langu, na boma langu,
na mwokozi wangu.
(K) Wewe Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana.
Bwana ndiye aliye hai;
Na ahimidiwe mwamba wangu;
Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu.
(K) Wewe Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana.
Ampa mfalme wake wokovu mkuu,
Amfanyia fadhili masihi wake,
Daudi na mzao wake hata milele.
(K) Wewe Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana.
Yn. 8: 12
Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana,
yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,
bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
Mt. 17: 14-20
Mtu mmoja alimjia Yesu, akampigia magoti, akisema, Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponva. Yesu akajibu, akasema. Envi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema, Mbona sisi hatukuweza ku- mtoa? Yesu akawaambia, Kwa sababu va upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
Maoni
Ingia utoe maoni