Masomo ya Misa
Sikukuu ya Mtakatifu Laurent, Mshahidi (Alhamisi, Agosti 10, 2017)
2Kor 9: 6-10
Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna sikuzote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele. Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atavaongeza mazao ya haki yenu.
Zab. 112: 1-2, 4, 9
Heri mtu yule amchaye Bwana,
Apendezwaye sana na maagizo yake.
Wazao wake watakuwa hodari duniani;
Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
(K) Heri atendaye fadhali na kukopesha.
Nuru huwazukia wenye adili gizani;
Ana fadhili na huruma na haki.
(K) Heri atendaye fadhali na kukopesha.
Amekirimu, na kuwapa maskini,
Haki yake yakaa milele,
Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
(K) Heri atendaye fadhali na kukopesha.
Yn 8: 12
Aleluya, aleluya,
Yeye anifuataye, asema Bwana, hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
Yn 12: 24-26
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi. Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Maoni
Ingia utoe maoni