Jumapili. 28 Aprili. 2024

Masomo ya Misa

KUMBUKUMBU YA WAT. YOAKIM NA ANNA, WAZAZI WA BIKIR (Jumatano, Julai 26, 2017)  

Somo la 1

Ybs. 44:1, 10 – 15

Haya na tuwasifu watu wa utauwa, Na baba zetu katika vizazi vyao. Lakini hawa walikuwa watu wa utauwa, wala kazi zao za haki hazisahauliki. Wema wao utawadumia wazao wao, Na urithi wao una wana wa wana; Wazao wao wanashikamana na agano, Na watoto wao kwa ajili yao. Kumbukumbu lao litadumu milele, Wala haki yao haifutiki kamwe; Miili yao imezikwa katika amani, Na jina lao laishi hata vizazi vyote. Mkutano wa watu wataitangaza hekima yao, Na makusanyiko watazihubiri sifa zao.

Wimbo wa Katikati

Zab. 132:11, 13 – 14, 17 – 18

Bwana amemwapia Daudi neno la kweli,
Hatarudi nyuma akalihalifu,
Baadhi ya wazao wa mwili wako
Nitawaweka katika kiti chako cha enzi.
(K) Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

Kwa kuwa Bwana ameichagua Sayuni,
Ameitamani akae ndani yake.
Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele,
Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani.
(K) Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

Hapo nitamchipushia Daudi pembe,
Na taa nimemtengenezea masihi wangu.
Adui zake nitawavika aibu,
Bali juu yake taji yake itasitawi.
(K) Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

Shangilio

Lk. 2:15

Aleluya, aleluya,
Waliitarajia faraja ya Israeli,
na Roho Mtakatifu alikuwa juu yao.
Aleluya.

Injili

Mt. 13:16 – 17

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.

Maoni


Ingia utoe maoni