Jumatatu. 20 Mei. 2024

Masomo ya Misa

Jumatano ya 13 ya Mwaka (Jumatano, Julai 05, 2017)  

Somo la 1

Mwa. 21:5, 8-20

Ibrahimu alikuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka. Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya. Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huko mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako. Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba. Yale maji yakaishaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja. Akaenda akakaa akimkabili, mbali i kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapazaza sauti yake, akalia. Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa. Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana. Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.

Wimbo wa Katikati

Zab. 34 : 6-7, 9-13

Maskini huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa na taabu zake zote.
Malaika wa Bwana hufanya kituo,
akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
(K) Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.

Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake,
yaani, wamchao hawahitaji kitu.
Wana-simba hutindikiwa, huona njaa,
bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu
chochote kilicho chema.
(K) Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.

Njoni, enyi wana, mnisikilize,
nami nitawafundisha kumcha Bwana.
Ni nani mtu yule apcndezwaye na uzima,
apendaye siku nyingi apate kuona mema?
(K) Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.

Shangilio

Zab. 119:105

Aleluya, aleluya,
Neno lako ni taa ya miguu yangu,
na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.

Injili

Mt. 8 :28-34

Yesu alipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja Kututesa kabla ya muhula wetu? Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe. Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini. Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote, na habari za wale wenye pepo pia. Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke mipakani mwao.

Maoni


Ingia utoe maoni