Jumatatu. 20 Mei. 2024

Masomo ya Misa

Jumanne ya 13 ya Mwaka (Jumanne, Julai 04, 2017)  

Somo la 1

Mwa. 19 :15-29

Hata alfajiri ndipo malaika walimhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyohurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako; usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa. Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi. Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari. Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana. Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waiiokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile. Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi. Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za Bwana, nave akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuru. Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.

Wimbo wa Katikati

Zab. 26:2-3,9-12

Ee Bwana, unijaribu na kunipima;
Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.
Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu,
Nami nimekwenda katika kweli yako.
(K) Fadhili zako, ee Bwana, zi mbele ya macho yangu.

Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji,
Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu.
Mikononi mwao mna madhara,
Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa.
(K) Fadhili zako, ee Bwana, zi mbele ya macho yangu.

Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu;
Unikomboe, unifanyie fadhili.
Mguu wangu umesimama palipo sawa;
Katika makusanyiko nifamhimidi Bwana.
(K) Fadhili zako, ee Bwana, zi mbele ya macho yangu.

Shangilio

Yn. 14:23

Aleluya, aleluya,
Mtu akinipenda, atalishika neno langu,
na Baba yangu atampenda,
na sisi tutakuja kwake.
Aleluya.

Injili

Mt. 8:23-27

Yesu alipanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. Wale watu wakamka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo na bahari zamtii?

Maoni


Ingia utoe maoni