Ijumaa. 17 Mei. 2024

Masomo ya Misa

Jumamosi ya 5 ya Pasaka (Jumamosi, Mei 20, 2017)  

Somo la 1

Mdo 16:1-10

Siku zile, Paulo alifika Derbe na Listra na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani. Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio. Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani. Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike. Makanisa yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku. Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. Walipofika kukabili Misia, wakajaribu kwenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, wakapita Misia wakatelemka Troa. Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Basi alipo- kwisha kuyaona vale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia. kwa kuwa tuliena hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.

Wimbo wa Katikati

Zab. 100 :1-3, 5

Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yole.
Mtumikieni Bwana kwa furaha.
Njoni mbelc zake kwa kuimba;
(K) Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote. au: Aleluya.


Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake:
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
(K) Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote. au: Aleluya.


Kwa kuwa Bwana ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi.
(K) Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote. au: Aleluya.

Shangilio

Yn. 20-29

Aleluya, aleluya,
Wewe Toma, umesadiki kwa kuwa umeniona, wa heri wale wasioona wakasadiki.
Aleluya,

Injili

Yn 15 : 18-21

Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.

Maoni


Ingia utoe maoni