Dominika ya 22 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 20:7-9Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 63:1-5, 7-8Ee Bwana, Mungu wangu, nafsi yangu inakuonea kiu.
Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu.
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na chovu, isiyo na maji.
K. Ee Bwana, Mungu wangu, nafsi yangu inakuonea kiu.
Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na utukufu wako.
Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai,
Midomo yangu itakusifu.
K. Ee Bwana, Mungu wangu, nafsi yangu inakuonea kiu.
Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai,
Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono,
Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
K. Ee Bwana, Mungu wangu, nafsi yangu inakuonea kiu.
Maana Wewe umekuwa msaada wangu,
Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
Nafsi yangu imekuandama sana,
Mkono wako wa kuume unanitegemeza.
K. Ee Bwana, Mungu wangu, nafsi yangu inakuonea kiu.
Somo la Pili
Rum 12:1-2Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Lk 21:36Kesheni kila wakati, ili mpate kuokoka,
na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.
Aleluya
Injili
Mt 16:21-27Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
TADEUS TLUWAY · 31 Agosti 2026
hakika 'mkatoliki leo' inatuunganisha na Mungu
Egrasius Salvatory · 3 Septemba 2026
Ndiyo