Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

JUmatano ya 25 ya Mwaka (Jumatano, Septemba 25, 2024)  

Somo la 1

Mit 30:5-9

Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwambinio. Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo. Mambo haya wawili nimekuomba; Usininyime kabla sijafa. Usiondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; unilishe chakula kilicho kadiri yangu. Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.

Wimbo wa Katikati

Zab 119:29, 72, 89, 101, 104, 163

Uniondolee njia ya uongo,
Unineemeshe kwa sheria yako.
Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu,
Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
(K) Neno lako nit aa ya miguu yangu.

Ee Bwana, neno lako lasimama,
Imara mbinguni hata milele.
Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya,
Ili nilitii neno lako.
(K) Neno lako nit aa ya miguu yangu.

Kwa mausia yako najipatia ufahamu,
Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
Nimeuchukia uongo, umenikirihi,
Sheria yako nimeipenda.
(K) Neno lako nit aa ya miguu yangu.

Shangilio

1Sam 3:9

Aleluya, aleluya,
Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia, wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Aleluya.

Injili

Lk 9:1-6

Yesu aliwaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa. Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili. Na nyumba yoyote mtakayoingia kaeni humo tokeni humo. Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung’uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao. Wakaenda, wakazunguka katika vijiji, wakihubiri Injili na kupoza watu kila mahali.

Maoni


Ingia utoe maoni