Masomo ya Misa
Alhamisi ya 15 ya Mwaka (Alhamisi, Julai 18, 2024)
Isa 26:7–9, 12, 16–19
Njia yake mwenye haki ni unyofu; wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki. Naam, katika njia ya hukumu zako sisi tumekungoja, Ee Bwana; shauku ya nafsi zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako. Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; maana hukumu zako zikiwapo duniani, watu wakaao duniani hujifunza haki. Bwana, utatuamuria Amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote. Bwana, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu ayko ilipokuwa juu yao. Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na utungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee Bwana. Tumekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumekuwa kana kwamba tumeza upepo; hakutkufanya wokovu wowote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani. Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
Zab 102:12–20
Wewe, Bwana, utaketi ukimiliki milele,
Na kumbukumbu lako kizazi hata kizazi.
Wewe mwenyewe utasimama,
Na kuirehemu Sayuni,
Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia,
Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.
Maana watumishi wake wameyaridhia mawe yake;
Na kuyaonea huruma mavumbi yake.
(K) Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana,
Na wafalme wote wa dunia utukufu wake.
Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana katika utukufu wake.
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau maombi yao.
(K) Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Kizazi kitakachokuja kitaandikia hayo,
Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.
Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na kuwafungua walioandikiwa kufa.
(K) Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Zab 111:7, 8
Aleluya, aleluya,
Maagizo yako yote, ee Bwana, ni amini, yamethibitika milele na milele.
Aleluya.
Mt 11:28–30
Yesu aliwaambia makutano: Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, name nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Maoni
Ingia utoe maoni