Masomo ya Misa
Dominika ya 21 ya Mwaka (Jumapili, Agosti 27, 2023)
Isa 22:19-23
Bwana, Bwana wa majeshi, asema hivi: Nami nitakusukuma na kukutoa katika mahali pako, naye atakushusha utoke hapa usimamapo. Na itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia; nami nitamvika vazi lako, nitamtia nguvu kwa mshipi wako, nami nitamkabidhi yeye mamlaka yako; naye atakuwa baba kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa nvumba ya Yuda. Na ufunguo wa nvumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga. Nami nitamkaza kanta msumari mahali palipo imara; naye atakuwa kiti cha utukufu kwa nyumba ya baba yake.
Zab 138: 1-3, 6, 9
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu.
(K) Ee Bwana, fadhili zako ni za milele, Usiziache kazi za mikono yako.
Nitalishukuru jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa maana umeikuza ahadi yako,
Kuliko jina lako lote.
Siku ile niliyokuita ulinitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
(K) Ee Bwana, fadhili zako ni za milele, Usiziache kazi za mikono yako.
Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu,
Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
Ee Bwana, fadhili zako ni za milele;
Usiziache kazi za mikono yako.
(K) Ee Bwana, fadhili zako ni za milele, Usiziache kazi za mikono yako.
Rum 11:33-36
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.
Mt 11:25
Aleluya, aleluya,
Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili. ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya
Mt 16:13-20
Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipo, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena Yohane Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaa- mbia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia. Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikufunulia hili, bali Baba vangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo.
Maoni
Ingia utoe maoni