Jumapili. 24 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Ijumaa ya 19 ya Mwaka (Ijumaa, Agosti 18, 2023)  

Somo la 1

Yos 24:1-13

Yoshua aliwakusanya kabila zote za Israeli huko Shekemu, akawaita wazee wa Israeli, na wakuu wao, na waamuzi wao, na maakida yao; nao wakahudhuria mbele za Mungu. Yoshua akawaambia watu wote: Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng’ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Ibrahimu, naye ni baba yake Nahori; wakaitumikia miungu mingine. Nami nikamtwaa Ibrahimu baba yenu toka ng’ambo ya Mto, nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani; nikaongeza uzao wake, nikampa Isaka. Kisha nikampa huyo Isaka Yakobo na Esau; nami nikampa Esau mlima Seiri aumiliki; Yakobo na watoto wake wakashuka Misri. Kisha nikawatuma Musa na Haruni, nikaipiga nchi ya Misri, kwa hayo yote niliyoyatenda kati yake; hatimaye nikawatoa ninyi. Nikawatoa baba zenu watoke Misri; nanvi mkaifikilia habari; Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka bahari ya Shamu. Nao walipomlilia Bwana, akaweka giza kati ya ninyi na Wamisri, akaileta bahari juu yao, akawafunikiza: navo macho yenu yaliyaona mambo niliyoyatenda huko Misri; kisha mkakaa jangwani siku nyingi. Kisha nikawaleta na kuwaingiza katika nchi ya Waamori, waliokaa ng’ambo ya pili ya Yordani: nao wakapigana nanyi; nikawatia mikononi mwenu. mkaimiliki nchi yao; nami nikawaangamiza mbele yenu. Ndipo Balaki, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, akainuka, akapigana na Israeli; tena akatuma watu akamwita Balaamu, mwana wa Beori, aje awalaani; lakini sikukubali kumsikiliza Balaamu: kwa hiyo akafuliza kuwabarikia ninyi; basi nikawatoa katika mkono wake. Nanyi mliuvuka Yordani, mkafika Yeriko; nao watu wa Yeriko wakapigana nanyi, Mwamori, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhiti, na Mgirgashi, na Mhivi, na Myebusi; nami nikawatia mikononi mwenu. Nikatuma mavu mbele yenu, waliowafukuza mbele yenu hao wafalme wawili wa Waamori, si kwa upanga wako, wala kwa upinde wako. Nami nimewapa ninyi nchi msiyoitendea kazi, na miji msiyoijenga, nanyi mmekaa humo; mnakula matunda ya mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.

Wimbo wa Katikati

Zab 136:1-4, 16-18, 21-22

Aleluya.
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Mshukuruni Mungu wa miungu;
kwa maana fadhili zake ni za milele.
(K) Maana fadhili zake ni za milele.

Mshukuruni Bwana wa mabwana,
kwa maana fadhili zake ni za milele.
Yeye peke yake afanya maajabu makuu,
kwa maana fadhili zake ni za milele.
(K) Maana fadhili zake ni za milele.

Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake,
kwa maana fadhili zake ni za milele.
Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
(K) Maana fadhili zake ni za milele.

Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Akawaua wafalme mashuhuri;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
(K) Maana fadhili zake ni za milele.

Akaitoa nchi yao iwe urithi;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Urithi wa Israeli mtumishi wake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
(K) Maana fadhili zake ni za milele.

Shangilio

2 Tim 1:10

Aleluya, aleluya,
Mwokozi wetu Yesu Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote. mkumshukuru Mungu Baba kwa Yeye.
Aleluya.

Injili

Mt 19:3-12

Mafarisayo walimwendea Yesu wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa. Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumobni mwa mama zao; tena wak omatowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

Maoni


Ingia utoe maoni