Jumapili. 24 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Alhamisi ya 8 ya Mwaka (Alhamisi, Juni 01, 2023)  

Somo la 1

Ybs 42: 15-25

Sasa nitayanena matendo ya Bwana, name nitayadhihirisha mambo yale niliyoyaona, kwa neon la Bwana vimekuwapo viumbe vyake, na kazi imependezayo ni sawasawa na amri yake. Jua litoapo nuru hudhihirika mahali pote; na kazi ya Bwana imejaa utukufu wake. Watakatifu wa Mungu hawawezi kuyatangaza maajabu na miujiza yake, walakini Mungu amewapa majeshi yake uwezo wa kusimama mbele ya utukufu wake. Yeye huchunguza vilindi, na moyo wa binadamu, na kuyayambua mashauri yake ya siri; kwa maana aliye juu amaizi yote yaliyo ujuzinaye hupenya ishara za ulimwengu, hutujulisha yaliyopita, na yatakayokuja, na kuzifunua alama za mambo yaliyofichwa. Hakuna wazo asilolijua, wala hakuna neon lo lote ambalo limefichwa naye. Matendo makuu ya hekima yake ameyaratibisha, ambaye, yeye ni mmoja tu, tangu milele na hata milele; hakuzidishiwa kitu, wala kupunguziwa kitu; wala yeye hana haja ye yote ya mshauri. We ajabu ya uzuri wa viumbe vyake, mtu angeweza kuliona hilo hata kwa habari ya cheche. Vitu vyote vyaishi na kudumu daima, na kwa kila haja vyote vyamtii. Vyote vinahitilafiana, wala hakufanya cho chote kisicho kamili; hata kimoja kinapita kingine kwa uzuri uzidio; naye ni nani atakayekinai kwa kuutazama utukufu wake?

Wimbo wa Katikati

Zab 33: 2-9

Mshukuruni Bwana kwa kinubi, kwa kinanda cha nyuzi kumi wmimbieni sifa.
Mwimbieni wimbo mpya, pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe.
(K) Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika.

Kwa kuwa neno la Bwana lina adili,
na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
Huzipenda haki na hukumu,
Nchi imejaa fadhili za Bwana.
(K) Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika.

Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika,
na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.
Hukusanya maji ya bahari chungu chungu,
Huviweka vilindi katika ghala.
(K) Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika.

Nchi yote na imwogope Bwana, wote wakaao duniani na wamche.
Maana yeye alisema, ikawa; nay eye aliamuru, ikasimama.
(K) Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika.

Injili

Mk 10: 46-52

Walifika Yeriko; Yesu alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia. Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu. Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita. Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani

Maoni


Ingia utoe maoni