Alhamisi ya 27 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Gal. 3:1 – 5Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Lk. 1:69 – 75Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake.
Ametusimamishia pembe ya wokovu
Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.
Kama alivyosema tangu mwanzo
Kinywa cha manabii wake watakatifu.
K. Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake.
Tuokolewe na adui zetu
Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;
Ili kuwatendea rehema baba zetu,
Na kulikumbu agano lake takatifu.
K. Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake.
Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yeu,
Ya kwamba atatujalia sisi,
Tuokoke mikononi mwa adui zetu,
Na kumwabudu pasipo hofu,
Kwa utakatifu na kwa haki
Mbele zake siku zetu zote.
K. Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake.
Shangilio la Injili
1 Pet. 1:25Neno la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.
Injili
Lk. 11:5-13Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nayi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au samaki, badala y asamaki atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni