Jumatatu. 28 Novemba. 2022

Masomo ya Misa

Jumatano ya 26 ya Mwaka (Jumatano, Septemba 28, 2022)  

Somo la 1

Ayu 9:1–12, 14–16

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, kweli najua kuwa ndiyvo hivyo; lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu? Kama akipenda kushindana naye, hawezi kumjibu neno moja katika elfu. Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yanke, naye akafanikiwa? Aiondoaye dunia itoke mahali pake,na nguzo zake kutetema. Aliamuruye jua, nalo halichomozi; nazo nyota huzipiga muhuri. Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu. Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari. Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hivyo kilima, na makundi ya nyota ya kusini. Atendaye mambo makuu yasiyotafutikana; naam, mambo ya ajabu yasiyohesabika. Tazama, yuaenenda karibu nami, nisimwone; tena yuapita kwenda mbele, nisitambue. Tazama, yuakamata, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwuliza, Wafanya nini? Je! Siuze mimi nitamjibuje, na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye? Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, nisingemjibu; nisingemsihi-sihi mtesi wangu. Kama ningemwita, naye akaniitikia hata hivyo nisingeamini kuwa ameisikia sauti yangu.

Wimbo wa Katikati

Zab 88:9–14

Bwana, nimekuita kila siku,
Nimekunyoshea Wewe mikono yangu.
Wafu je! Utawafanyia miujiza?
Au waliofariki watasimama na kukuhimidi?
(K) Maombi yangu yafike mbele zako, Ee Bwana.

Fadhili zako zitasimuliwa kaburini?
Au uaminifu wako katika uharibufu?
Miujiza yako itajulikana gizani?
Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?
(K) Maombi yangu yafike mbele zako, Ee Bwana.

Lakini mimi nimekulilia Wewe, Bwana,
Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.
Bwana, kwa nini kuitupa nafsi yangu,
Na kunificha uso wako?
(K) Maombi yangu yafike mbele zako, Ee Bwana.

Shangilio

Mt 4:4

Aleluya, aleluya,
Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Aleluya.

Injili

Lk 9:57-62

Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja alimwambia, Nitakufuata kokote utakakokwenda. Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana vioto, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake. Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusu kwanza niende nikamzike baba yangu. Akamwambia, Waache wafu wawazike wafu; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu. Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusu kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.

Maoni


Ingia utoe maoni