Jumamosi. 27 Aprili. 2024

Masomo ya Misa

Alhamisi ya 19 ya Mwaka (Alhamisi, Agosti 11, 2022)  

Somo la 1

Eze 12:1–12

Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Mwanadamu, wewe unakaa katika ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi. Basi, mwanadamu, funga tayari vyombo kwa uhamisho, ukahame wakati wa mchana mbele ya macho yao; nawe utahama toka mahali pako hapa mpka mahaoli pengine mbele ya macho yao; labda watafahamu, wajapokuwa ni nyumba iliyoasi. Nawe ukatoa vyombo vyako, wakati wa mchana, mbele ya macho yao, kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa; nawe mwenyewe utatoka, wakati wa jioni, mbele ya macho yao, kama watu watokavyo katika kuhamishwa. Toboa mahali ukutani mbele ya macho yao, kama watu watokavyo katika kuhamishwa. Toboa mahali ukutani mbele ya macho yao, ukachukue vitu kwa kuvipitisha pale. Mbele ya macho yao utajitwika begani pako, na kuvichukua nje gizani; utafunika uso wako, hata usiione nchi; kwa maana nimekuweka uwe ishara kwa nyumba ya Israeli. Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nalitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavito agizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao. Asubuhi neno la Bwana likanijia, kusema, Mwanadamu, nyumba ya Israeli, je! Nyumba ile iliyoasi, hawakukuambia, Unafanya nini wewe? Waambie Bwana Mungu asema hivi; Ufunuo huu wamhusu mkuu wa Yerusalemu, na nyumba yote ya Israeli walio kati ayo. Sema, Mimi ni ishara kwenu; kama mimi nilivyotenda, wao nao watatendwa vile vile; watahamishwa, watakwenda kufungwa. Naye mkuu aliye kati yao atachukua begani katika giza; naye atatoka kwenda zake; watatoboa mahali ukutani, wapate kuvichukua vyombo vyao nje; atafunika uso wake, kwa sababu hataiona nchi kwa macho yake.

Wimbo wa Katikati

Zab 78:56–59, 61–62

Walimjaribu Mungu Aliye juu wakamwasi.
Wala hawakuzishika shuhuda zake.
Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao;
Wakaepea kama upinde usiofaa.
(K) Usiyasahau matendo ya Mungu.

Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu,
Wakamtia wivu kwa sanamu zao,
Mungu akasikia, akaghadhibika,
Akamkataa Israeli kabisa.
(K) Usiyasahau matendo ya Mungu.

Akaziacha nguvu zake kutekwa,
Na fahari yake mkononi mwa mtesi.
Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga;
Akaughadhibikia urithi wake.
(K) Usiyasahau matendo ya Mungu.

Shangilio

Kol 3:16, 17

Aleluya, aleluya,
Neno la Kristu likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote; mkimshukuru Mungu Baba kwa Yeye.
Aleluya.

Injili

Mt 18:21–19:1

Petro alimwendea Yesu akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipowe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa waojli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake. Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng’ambo ya Yordani.

Maoni


Ingia utoe maoni