Jumatano. 27 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Jumatano ya 11 ya Mwaka (Jumatano, Juni 17, 2020)  

Somo la 1

2Fal 2:1, 6-14

Bwana alipopenda kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha. Eliya akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana bwana amenituma niende mpaka Yordani. Akasema, kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Wakaendelea mbele wote wawili. Basi watu hamsini wa wale wana wa manabii wakaenda wakasimama, kuwakabili kwa mbali; na hao wawili wakasimama karibu na Yordani. Eliya akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja, akayapiga maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka pakavu. Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lolote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu. Akasema, Umeomba neno guvu; lakini, ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la, hukuniona, hulipati. Ikawa walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kutatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli. Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa; akashika mavazi yake mwenyewe, akayararua vipande viwili. Kisha akaliokota lile vazi la Eliya lililomwangukia, akarudi, akasimama katika ukingo wa Yordani. Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye laipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka. Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye laipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka.

Wimbo wa Katikati

Zab 31:19, 20, 23

Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako
Ulizowawekea wakuchao;
Uulizowatendea wakukimbiliao
Mbele ya wanadamu!
(K) Iweni hodari, mpige moyo konde, ninyi nyote mnaomngoja Bwana.

Utawasitiri na fitina za watu
Katika sitara ya kuwapo kwako.
(K) Iweni hodari, mpige moyo konde, ninyi nyote mnaomngoja Bwana.

Mpendeni Bwana,
Ninyi nyote mlio watauwa wake.
Bwana huwahifadhi waaminifu,
Humlipa atendaye kiburi malipo tele.
(K) Iweni hodari, mpige moyo konde, ninyi nyote mnaomngoja Bwana.

Shangilio

1Pet 1:25

Aleluya, aleluya,
Neno la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.

Injili

Mt 6:1-6, 16–18

Yesu aliwaambia wanafunzi wake; Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Basli wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Tena mfungapo, msiwe kama wanfiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao; ili waonekane na watu kuwa nafunga, Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Maoni


Ingia utoe maoni