Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Dominika ya 12 ya Mwaka (Jumapili, Juni 19, 2016)  

Somo la 1

Zek 12:10-11

Bwana asema: Nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.

Wimbo wa Katikati

Zab 63:1-5, 7-8

Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
(K)Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu.

Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako.
Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.
(K)Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu.

Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
(K)Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu.

Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
Nafsi yangu inakuandama sana; Mkono wako wa kuume unanitegemeza.
(K)Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu.

Somo la 2

Gal 3:26-29

Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Shangilio

Yn 6:63, 68

Aleluya, Aleluya
Bwana, maneno yako ni roho tena ni uzima; Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Aleluya

Injili

Lk 9:18-24

Yesu alipokuwa akisali kwa faragha, wanafunzi wake walikuwapo pamoja naye, akawauliza, Je! Makutano hao wanasema ya kuwa mimi ni nani? Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka. Akawaambia, Nanyi mwasema ya kwamba mimi ni nani? Petro akamjibu akasema, Ndiwe Kristo wa Mungu. Akawaonya, akawakataza wasimwambie mtu neno hilo; akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka. Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. alipokuwa akisali kwa faragha, wanafunzi wake walikuwapo pamoja naye, akawauliza, Je! Makutano hao wanasema ya kuwa mimi ni nani? Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka. Akawaambia, Nanyi mwasema ya kwamba mimi ni nani? Petro akamjibu akasema, Ndiwe Kristo wa Mungu. Akawaonya, akawakataza wasimwambie mtu neno hilo; akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka. Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.

Maoni


Ingia utoe maoni