Masomo ya Misa
Jumatatu ya 20 ya Mwaka (Jumatatu, Agosti 19, 2019)
Amu 2: 11-19
Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali. Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika. Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye ikawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui ao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao. Kila walikokwenda, mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana. Kisha Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara. Lakini nawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana; bali wao hawakufanya hivyo. Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua. Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao. kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi.
Zab 106: 34-37, 39-40, 43-44
Hawakuwaharibu watu wa nchi
Kama Bwana alivyowaambia;
Bali walijkhanganya na mataifa,
Wakajifunza matendo yao.
(K) Ee Bwana, unikumbuke mimi, kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Wakazitumikia sanamu zao,
Nazo zikawa mtego kwao.
Naam. walitoa wana wao na binti zao
Kuwa dhabihu kwa mashetani.
(K) Ee Bwana, unikumbuke mimi, kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao,
Wakafanya uasherati kwa matendo yao.
Hasira ya Bwana ikawaka juu ya watu wake,
Akauchukia urithi wake.
(K) Ee Bwana, unikumbuke mimi, kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Mara nyingi aliwaponya,
Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao,
Wakadhilika katika uovu wao.
Lakini aliyaangalia mateso yao,
Aliposikia kilio chao.
(K) Ee Bwana, unikumbuke mimi, kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
1 Thes 2:13
Aleluya, aleluya,
Lipokeeni neno la Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu.
Aleluya
Mt 19:16-22
Mtu mmoja alimwendea Yesu akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Lsishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena? Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Maoni
Ingia utoe maoni