Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Masomo ya Misa

Jumatano ya 7 ya Mwaka (Jumatano, Mei 18, 2016)  

Somo la 1

Yak 4:13-17

Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya. Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

Wimbo wa Katikati

Zab 49:1-2,5-10


Sikieni haya, enyi mataifa yote; Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani.
Watu wakuu na watu wadogo wote pia, Tajiri na maskini wote pamoja.
(K)Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao

Kwa nini niogope siku za uovu, Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?
Wa hao wanaozitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao;
(K)Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao

Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,
(Maana fidia ya nafsi zao ina gharama, Wala hana budi kuiacha hata milele;)
ili aishi sikuzote asilione kaburi.
(K)Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao

Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa;
Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao.
(K)Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao

Shangilio

Yn 14:6


Aleluya, Aleluya
Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima;asema Bwana
Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Aleluya

Injili

Mk 9:38-40

Yohana akamjibu Yesu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi. Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya; kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.

Maoni


Ingia utoe maoni