Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni amemteua Askofu mkuu Luigi Bianco kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uganda. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Balozi wa Vatican huko Ethiopia, Djibouti na Mwakilishi wa Kitume nchini Somalia. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Luigi Bianco alizaliwa kunako tarehe 3 Machi 1960 huko Montemagno, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, tarehe 30 Machi 1985 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, huko Casale Monferrato, Italia.
Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, tarehe 12 Januari 2009 akamteuwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 25 Aprili 2009 na Kardinali Tarcisio Bertone. Akatumwa kwenda Honduras kama Balozi wa Vatican. Tarehe 12 Julai 2014, akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Ethiopia na tarehe 10 Septemba, akaongezewa tena utume huko nchini Djibouti. Tarehe 10 Septemba 2014, akateuliwa na Papa Francisko kuwa Mwakilishi wa Kitume huko nchini Somalia. Mwishoe, Baba Mtakatifu Francisko tarehe 4 Februari 2019 akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uganda.
Maoni
Ingia utoe maoni