Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 13 Februari 2019 amekutana na kuzungumza na Bwana Brad Smith, Rais wa Kampuni ya Microsoft, aliyekua ameambatana na Askofu mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha na Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo II. Katika mazungumzo yao na Baba Mtakatifu, wamegusia kuhusu “artificial intelligence” yaani “akili bandia” kwa ajili ya huduma ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Wameongelea juu ya mchakato wa kujenga daraja katika ulimwengu wa kidigitali, ili kurekebisha pengo kubwa lililopo duniani.
Mwishoni mwa mazungumzo yao, Bwana Brad Smith amemwambia Baba Mtakatifu Francisko kwamba, kwa kushirikiana na Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha, wameamua kuanzisha “Tuzo ya Maadili Katika Matumizi ya Akili Bandia”, tema itakayojadiliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha kwa mwaka 2020. Mkutano mkuu wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha utafanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 25-27 Februari 2019, kwa kuongoza na kauli mbiu “Maadili ya Roboti, Binadamu, Mashini na Afya”.
Maoni
Ingia utoe maoni