Jumamosi. 23 Novemba. 2024
feature-top
Katika kuelekea Siku ya Radio Duniani,Unesco inahamasisha kufungua Radio nyumbani,katika gari au simu ya mkono na mahali popote kusikiliza

Kilele cha Siku ya Radio duniani ni tarehe 13 Februari 2019,inayoongozwa na mada ya mazungumzo,uvumilivu na amani.Shirika la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO) linahamasisha kufungua Radio nyumbani,katika gari au simu ya mkono ili kuenzi chombo hiki maalum ambacho kimesikindikiza maisha katika historia

Tunapokaribia kilele cha Siku ya Radio duniani tarehe 13 Februari inayoongozwa mwaka huu na kauli mbiu mazungumzo, uvumilivu na amani, shirika Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) linahamasisha kufungua Radio nyumbani, katika gari au simu ya mkono ili kuweza kusheherekea siku hii ambayo inatazama kwa chombo hiki maalum ambacho kimesikindikiza maisha yetu katika historia.

UNESCO inahamasisha vituo vya radio na mashirika kutoa umuhimu wa kuheshimu tofauti

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO lilianzisha Siku ya Radio Duniani kunako mwaka 2012 mara baada ya Baraza Kuu la Unesco kutambua umuhimu wake na mwaka uliofuata Umoja wa Mataifa ukatambua kama Siku ya Radio duniani. Hata hivyo kwa kuthibitisha kuwa, kila tarehe 13 Februari itakuwa inaadhimishwa kutokana na kwamba, tarehe hiyo mwaka 1946 ndipo ilianzishwa Radio ya Umoja wa Mataifa. Ni katika kutumia chombo hiki cha mawasiliano na msingi wa kutoa habari ambayo inasaidia kukuza uhuru wa kujieleza na usawa wa kila kitu. Radio iweze kutoa mchango katika mijadala ya kidemokrasia kwa njia ya kubadilishana mawazo kati ya watangazaji na wasikilizaji. Kwa maana hiyo Radio imekuwa ni nguzo kuu ya kijamii inayoendelea na iliyo endelea duniani kote.

Mada ya siku hii imejikita kuanzishwa kwa mambo mengi duniani kama vile barani Asia, Afrika, Amerika na Ulaya katika siku hii ambayo inaongozwa na kauli mbiu mazungumzo, kuvumilia na amani. Katika lengo hilo,Unesco inaalika vituo vyote vya Radio na mashirikisha yote ya kidini na uma kuunga mkono katika kuhamasisha kwa wasilikizaji, umuhimu wa kuheshimu tofauti na juhudi zaidi kwa ajili ya amani na maendeleo. Katika kuelezea umuhimu wa siku hii, Unesco inasistiza kuwa, Radio inafundisha, inabadilisha na kuunganishwa watu na jumuiya za kila kona duniani katika kuhamasisha na kukuza mazungumzo  hai ya kuweza kuleta mabadiliko chanya kijamii. Ni katika kuanzia katika radio, ambayo ni chombo madhubuti na dhati kinaweza kabisa kupinga vikali michakato ya vurugu, usambazwaji wa migogoro hasa katika kanda mbalimbali ambazo zimegubikwa na hali halisi hiyo ili katika mazungumzo chanya yaweze kuleta amani kati ya watu.

Tarehe 13 Februari, Radio zote zitoe fursa ya vipindi vya kutafakari mada ya Siku ya Radio duniani

Katika misingi hii, Siku ya Radio duniani mwaka 2019 inawaalika kwa nguvu zote kuwa na jitihada za kila mmoja iwezekanavyo ili kusaidia kukuza mazungumzo, uvumilivu na amani. Wito wa UNESCO kwa Radio zote dunia ni ile ya kuweza kuacha  nafasi zadi katika siku ya tarehe 13 Februari vipindi vingi vikwa vya majadiliano kati ya watangazaji na wasikilizaji. Wakati wa Siku hii, UNESCO inashauri kwamba radio kwa kupitia vipindi vyao na mahojiano vinaweza kuwasaidia wasikiliza kujua matukio mbalimbali na kuchangia kujua sababu kwa ujumla ambazo zinasaidia kuelimisha afya, jinsia, usawa na ushirikishwaji wa wahamiaji, au vurugu dhidi ya wanawake, wakati huo huo kuchangia kukuza ulewa zaidi wa umma habari zaidi za kijamii. Na ili kuweza kufanikisha mazungumzo, Unesco inawaomba radio zote duniani kushiriki maadhimisho kwa mfano kukaribisha wageni katika studio ili kufanya mijadala ya moja kwa moja ambayo inawaunganisha wasikilizaji wote ili kutoa ushuhuda na kuhamasisha matendo ya dhati katika roho ya uvumilivu na Amani!

Kwa njia hiyo tarehe 13 Februari katika Radio zote wanaomba vipindi visiwe vya muziki  zaidi au matamasha, badala yake wajikite kwa dhati katika  mada muhimu sana za kujadili na ambazo kwa sasa kila siku zinaingia masikioni na zinahitaji umakini zaidi kama mwanga wa  kauli mbiu ya mwaka huu! Tangu UNESCO ianzishwe, imekuwa mstari wa mbele katika historia yake ya kuhimiza amani duniani kupitia elimu, sayansi na utamaduni. Juhudi za UNESCO za kulinda amani ya duniani inawezekana kwa pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ili kushirikiana katika kupambana na ugaidi, ukosefu wa uvumilia na ili kujenga dunia nzuri kwa njia ya kuendeleza elimu, sayansi na utamaduni lengo kuu ni kuona wanafikia mazungumzo ya kweli, ya uvumilivu na amani.

Radio duniani ni muhimu sana kwa kusaidia mawasiliano na ushirikiano

Siku ya Radio Duniani ni muhimu sana kwa sababu ya utambuzi wake kama chombo madhubuti cha mawasiliano ambayo yanasaidia ushirikiano kimataifa na vituo vya radio katika kutoa ujasiri wa kuunda mitandao na jumuiya katika kukuza usambazaji wa mawasiliano; uhuru wa kujieleza na mambo yote kwa ujumla katika masafa ya radio. Na zaidi kuna mchango mkubwa wa radio katika majadiliano ya kidmokrasia kwa njia ya mafunzo na ushirikishwaji kwa wasikilizaji wote. Hata hivyo Radio kama chombo maalum cha mawasiliano, inakumbukwa pia tarehe 29 Septemba 2018, Vyombo vya Habari Vatican vilitangaza kauli mbiu iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya Siku ya Mawasiliano duniani 2019, ambayo itaongozwa na maneno ya Mtakatifu Paulo kwa Waefeso yasemayo:kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa mwingine (Ef 4,25). Kutoka katika jamii hadi Jumuiya.

Msemaji wa Vyombo vya habari akifafanua kuhusiana na kauli mbiu hiyo alisema, inasisitiza umuhimu wa kurudisha mawasiliano kwa mtazamo mpana na inajikita katika msingi wa mtu na kusisitizia thamani ya mwingiliano unaolenga daima mazungumzo na kama fursa ya kukutana na mwingine”. Kwa kutazama kilele cha Siku ya Radio Duniani, inayoongozwa na mada ya mazungumzo, uvumilivu na amani ni wazi kwamba chombo hiki cha Radio ni madhubuti katika kutoa mchango mkubwa sana wa kuunganisha, na ambacho kinaweza kuleta manufaa kwa wote iwapo kweli kutakuwa na uwajibikaji wa uhuru wa kuzungumza, kuvumiliana na kuwa na amani. Tusikilize Radio ili tupate kuelimishwa na kuwa na utambuzi wa dunia yetu inakwenda vipi.



Maoni


Ingia utoe maoni