Alhamisi. 21 Novemba. 2024
feature-top
Mtakatifu Josephine Bakhita aliyekuwa mwathirika wa utumwa

Baba Mtakatifu ametoa wito kwa serikali kuthibiti biashara ya binadamu na utumwa na kuwalinda wathirika na wakati huo amesali na waamini sala ya Mtakatifu Bakhita,kwamba asaidie wale wote walioangukia katika mtego wa utumwa.Ni mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 10 Februari 2019

Siku mbili katika kumbukumbu ya Mtakatifu Josephine Bakhita ni mwaka  wa tano wa Siku ya kupinga  Biashara ya binadamu na utumwa. Kauli mbiu ya mwaka huu ni  pamoja dhidi ya kupinga biashara. Kwa pamoja tupinge biashara na tusishau hilo! Ni mwanzo wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko,Jumapili  tarehe 10 Februari 2019  mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, akikimbusha Siku hii muhimu ya kupinga biasha ya Utumwa ambayo inaadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 Februari yak ila mwaka,sambamba na kumbukumbu ya liturujia  ya Mtakatifu Josphine Bakhita ambaye ni mwathirika wa utumwa.

Akiendelea Baba Mtakatifu kuhimiza maana ya siku hii,anawaalika kuunganisha nguvu zote ili kushinda changamoto hii. Anawashukuru wadau wote ambao wanajikita kupambana na janga hili kwa namna ya pekee wamewataja watawa. Ametoa wito maalum kwa serikali zote duniani ili waweze kukabiliana na maamuzi ya sababu zinzosababisha janga hili,na pia wapate kuwalindwa waathirika wa utumwa. Aidha anasema kuwa lakini kwa wote inawezekana na lazima kushirikiana katika kutoa taarifa za kesi za unyanyaswaji na utumwa wa wanaume,wanawake na watoto. Baba Mtakatifu ameongeza kusema kwamba, sala ni nguvu inayosaidia katika jitahada za pamoja na kwa maana hiyo ameaalika kusali kwa pamoja, sala ya Mtakatifu Josephine Bakhita ambayo ilikuwa imesambazwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na kwa wote wamesali…

Sala ya Mtakatifu Bakhita: Mtakatifu Bakhita ukiwa mtoto wa miaka 6 uliuzwa kama mtumwa na ukaweza kukabiliana na matatizo na mateso yasiyoelezeka. Mara baada ya kukumbolewa kimwili,ulipata ukombozi wa kweli kwa kukutana na Kristo na Kanisa lake. Mtakatifu Bakhita,tuwasaidie wote walioangukia  katika mtego wa utumwa. Kwa jina lao uwaombee kwa Mungu wa huruma,ili minyororo ambayo imewafunga iweze kukatika. Mungu aweza kuwakumboa wote ambao wako hatarini, wamejeruhiwa au wananyanyaswa na utumwa na biashara ya binadamu. Leta faraja kwa wale ambao wameweza kukombolewa kutoka utumwani na uwafundishe watazame Yesu kama mfano wa imani na matumaini, kwa kufanya hivyo wanaweza kuponya majeraha yao. Tunakuomba usali na kutuombea sisi sote,ili tusiangukie katika utofauti, kwa sababu tunaweza kufungua macho ili kutazama suruba na majeraha ya kaka na dada wanaokosa hadhi yao na uhuru wao na uwasikilize kilio chao Amina. Mtakatfu Josephine Bakhita utumbee.

Mara baada ya sala hiyo amewasalimia mahujaji wote waliofika toka pande zote za dunia na kuwatakia Jumapili njema lakini wasisahalu kusali kwa ajili yake.


Maoni


Ingia utoe maoni