Jumanne. 03 Desemba. 2024
feature-top
Papa Francisko anawapongeza waamini wa Kanisa la Kiorthodox la Kikoptik la Misri kwa ushuhuda wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake!

Sherehe za Fumbo la Kuzaliwa Kristo Yesu, Mfalme wa amani, ziwe ni chemchemi ya amani, utulivu, ustawi na maendeleo nchini Misri, Mashariki ya Kati na ulimwengu katika ujumla wake. Baba Mtakatifu amepeleka salam maalum kwa Patriaki Tawadros II, ambaye katika utume wake, amekuwa kweli ni mfano bora wa kuigwa katika imani na mapendo, hata wakati wa nyakati tete!

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Mkesha wa Noeli kwa Makanisa ya Kiorthodox ametuma salam na matashi mema kwa njia ya video kwa waamini wa Kanisa la Kiorthodox la Kikoptik nchini Misri, kama sehemu ya uzinduzi wa Kanisa kuu la Kuzaliwa Bwana, huko Alexandria nchini Misri. Tukio hili limehudhuriwa na Patriaki Tawadros II pamoja na Rais Abdel Fattal al Sisi wa Misri. Baba Mtakatifu katika ujumbe wake, amewapongeza waamini wa Kanisa la Kiorthodox la Kikoptik nchini Misri kwa mfano na ushuhuda wa imani thabiti kwa Kristo Yesu na Kanisa lake.

Sherehe za Fumbo la Kuzaliwa Kristo Yesu, Mfalme wa amani, ziwe ni chemchemi ya amani, utulivu, ustawi na maendeleo nchini Misri, Mashariki ya Kati na ulimwengu katika ujumla wake. Baba Mtakatifu amepeleka salam maalum kwa Patriaki Tawadros II, ambaye katika maisha na utume wake, amekuwa kweli ni mfano bora wa kuigwa katika imani na mapendo, hata wakati wa nyakati tete katika maisha na utume wa Kanisa.

Ushuhuda wa wafiadini na waungama imani unawatia shime waamini kusonga mbele kwa imani na matumaini. Amewasalimia pia viongozi wa Serikali chini ya uongozi wa Rais Abdel Fattal al Sisi. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, sala na ibada zitakazotolewa na waamini katika Kanisa hili zipae kwenda mbinguni na neema ya Mungu iwashukie na kukaa na watu wake. Wachunguzi wa mambo wanasema, hili ni tukio muhimu la umoja na mshikamano wa familia ya Mungu nchini Misri katika mchakato wa majadiliano ya kidini na kiekumene kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Maoni


Ingia utoe maoni