Asilimia 70% ya watu milioni 9,6 wanakufa duniani kwa sababu ya saratani,hasa katika nchi zenye kipato cha chini. Saratani ya shingo la kizazi inashambulia kila mwaka wanake 500,000 duniani na wanawake 6,200 ni katika nchi ya Ethiopia, mahali ambapo Shirika la Madaktari na Afrika CUAMM wanajikita kwenye harakati za kukinga ugonja huo hadi hatua ya mwisho. Katika fursa ya kuadhimisha Siku ya kuthibiti saratani duniani, inayofanyika kila mwaka tarehe 4 Februari, Madaktari na Afrika (CUAMM) katika ripoti yao wanatoa wito ili kuweza kuwa makini juu ya tatizo ambalo hata barani Afrika, wagonjwa wa saratani bado ni wengi, ambao inakuwa vigumu kupata tiba inayostahili. Ukosefu wa uhamasishaji wa mada hii ni moja ya sababu msingi za kuendelea kubaki nyuma na ugojwa usiotibija katika bara hata kama kuna mitindo ambayo inaonesha kupiga hatua kwa kulenga zaidi juu ya kuzuia kwa kutumia vipimo na mionzi, lakini hata mahitaji ya mifumo mipya ya kisasa kwa mujibu wa ripoti ya CUAMM.
Saratani ni sababu ya pili ya vifo leo hii duniani
Kwa mujibu wa ripoti inathibitisha kwamba,Saratani leo hii ni sababu ya pili ya vifo duniani, kwani inakadhiriwa kuwa milioni 9,6 ya watu wanakufa kila mwaka. Asilimia 70 % ya nchi hizo ni zenye kipato cha chini. Wakati robo tatu ya mtindo wa kawaida wa saratani unawezekana kuzuiwa. Inakadiriwa milioni 3,7 wa watu wanaweza kukombolewa maiasha yao kila mwaka kwa kutumia rasilimali za kuunda mikakati ya kuzuia, kupima na kutibu kwa haraka. Mfano wa dhati ni saratani ya shingo ya kizazi, ambayo ni kati ya mtindo wa saratani kwa wanawake wengi duniani, ambapo kesi mpya ni 570 na 311 wanakufa kila mwaka. Na huo ndiyo mtindo wa aina ya pili wa saratani ambao umesambaa sasa katika nchi ya Ethiopia. Katika nchi hiyo, Madaktari na Afrika CUAMM wanaendeleza mbele mipango wa tiba ya mionzi katika Kanda ya Omo, Kaskazini mwa nchi mahali ambamo wanaishi wachungaji. Kwa ushirikiano na wakuu wa Afya mahalia wamewezesha kutengeneza vituo vya afya 14 vyenye uwezo wa mionzi na tiba. Kwa mujibu wa juhudi za Madaktari na Afrika CUAMM wanawake 3,500 wameweza kufika kupima na wamewezesha kufanya kampeni 21 za uhamasishaji ili kuwafundisha wahudumu 50 wa vituo vya afya mahalia waweze kukabiliana kwa kutambua namna ya kuwasaidia katika aina hii ya saratani. Vituo vya afya na wahudumu waliohusishwa,pia wamezawezesha kupatiwa vifaa muhimu kwa ajili ya shughuli zao ambazo zinahusiana na kupima wanawake kufanya uchunguzi wa afya zao na ikiwa wanagundua saratani wananaza tiba kwa haraka kwa maana ni muhimu kuanza mapema iwezekanavyo!
Ni miaka 51 sasa tangu kuanzishwa Chama cha Madaktari na Afrika
Kwa miaka 51 sasa tangu kuanzishwa kwa Chama cha Madaktari kwa ajili ya Afrika, CUAMM, kimekuwa ni kama sehemu ya mchakato wa kupambana na magonjwa yanayoendelea kudhalilisha utu na heshima ya binadamu pamoja na kuwatumbukiza watu katika umaskini na majanga mbali mbali ya maisha. CUAMM imekuwa ikishirikiana kwa karibu sana na Wizara ya Afya katika nchi husika kwa ajili ya kuweza kuboresha maisha ya jamii kwa ushirikiano na wizara za afya mahalia. CUAMM ilianzishwa kunako mwaka 1950 nchini Italia ambapo kimekuwa mstati wa mbele kujielekeza katika huduma bora, makini, ustawi na maendeleo ya jamii barani Afrika. Chama hiki cha Madaktari kinajihusisha na utekelezaji wa malengo ya muda mfupi na mrefu katika huduma ya afya, ili kuhakikisha kwamba, wananchi wanapata huduma bora ya afya, inayoweza kufikiwa na watu wengi zaidi. Leo hii CUAMM inatoa huduma yake katika nchi 8 Afrika chini ya jangwa la sahara kama vile (Angola, Etiopia, Musumbiji,Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Sierra Leone, Sudan ya Kusini, Tanzania, Uganda) wakiwa na zaidi ya wahudumu 2,200 wakiwa ni pamoja na wa Ulya na Afrika; mahospitali 24, vituo vya zahanati vidogo, vyenye kuhudumia raia mama na mtoto, mapambano ya virus vya ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na mafunzo. Vyuo 3 vya manesi na Chuo Kikuu kilichopo nchini Msumbiji.
Ugonjwa wa saratani ni kati ya magonjwa yanayoendelea kusababisha vifo vya watu wengi duniani. Shirika la Afya Duniani, WHO, linakadiria kwamba, takribani ya watu milioni themanini wanaweza kupoteza maisha yao kutokana na ugonjwa wa Saratani kati ya mwaka 2005 hadi kufikia mwaka 2015, kama hatua madhubuti hazitachukuliwa dhidi ya ugonjwa wa saratani ulimweguni. Huu ni ugonjwa ambao kwa sasa hauna ubaguzi tena, kwani wakati fulani baadhi ya watu walidhani kwamba, Saratani ni ugonjwa wa matajiri tu, lakini sasa gharama na madhara yake ni makubwa hata kwa nchi maskini duniani. Hii ni changamoto kwa wadau mbali mbali kusimama kidete kuhakikisha kwamba, mbinu madhubuti zinachukuliwa ili kudhibiti ugonjwa wa Saratani duniani.
Historia ya Siku ya Saratani duniani
Ilikuwa ni tarehe 4 Februari 2000 ambapo wakuu wa Jumuiya ya Kimataifa walikutana mjini Paris ili kuweka mkakati wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Saratani duniani na kuthibitisha kuwa kila ifikapo tarehe 4 Februari ya kila mwaka, Jumuia ya kimataifa itakuwa inaadhimisha Siku ya Saratani duniani, ambapo hii ni changamoto kwa wataalam, wafanyakazi katika sekta ya afya, wagonjwa, serikali, viwanda vya madawa na vyombo vya habari kuunganisha nguvu zake, ili kupambana na ugonjwa wa Saratani. Shirika la Afya Duniani, linapenda kuitumia tarehe 4 Februari ya kila mwaka, ili kuwahamasisha watu wafahamu ugonjwa wa saratani, matibabu yake, madhara yake pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha hali ya maisha ya wagonjwa wa Saratani. Katika harakati za Umoja wa mataifa na malengo mkakati waliyo kuwa wamejiwekea mwaka 2000 ilikuwa ni kuona kwamba wanapunguza maambukizi ya saratani kufikia mwaka 2020.
Kuzuia saratani
Wataalam wa masuala ya afya wanasema kwamba, walau asilimia 80% hadi 40% ya ugonjwa wa saratani unaweza kuzuiwa ikiwa kama watu watajenga utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara; kuhakikisha kwamba, wanapata chanjo zinazotakiwa kwa wakati muafaka; kujikinga na mionzi mikali ya jua; kula kwa wingi mboga za majani, kufanya mazoezi ya viungo, kupunguza uzito pamoja na kujenga mazoea ya kuchunguza afya yao wenyewe hasa akina mama kuhusiana na Saratani ya matiti. Shirika la afya duniani, WHO linasisitiza kuwa karibu kila familia duniani inaguswa na saratani kwa njia moja au nyingine lakini wakati huu kuna maendeleo fulani ambayo yamepatikana kuhusu tiba ya saratani. Licha ya hivyo WHO inasema mbali ya kupatikana maendeleo katika juhudi za kuzuia, kutibu na kutoa tiba kwa wagonjwa wa saratani, lakini maendeleo hayo hayapatikani duniani kote hivyo inabidi kuongeza juhudi zaidi ya kuhamasisha utamaduni wa kuchunguza mapema afya.
Maoni
Ingia utoe maoni