Jumatano. 04 Desemba. 2024
feature-top
Maandamano ya mawakili nchini Zimbawe kwa kudai haki ya waandamaji waliowekwa mbaloni hivi karibuni

Maaskofu katoliki nchini Zimbabwe wanashutumu vikali ghasia na ukiukwaji wa haki za binadamu,kufuatia na maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta ambapo maelfu ya watu wamewekwa mbaloni

Tumekutana ili kwa pamoja kuweza kujua ni kwa namna gani serikali na Kanisa, vinaweza kushirikiana kwa pamoja ili kutatua hali hii na ndiyo  mwanzo wa mchakato. Ndiyo uthibitisho wa Padre Fredrick Chiromba, katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Zimbabwe akielezea kuhusu mkutano wa wawakilishi wa Baraza la maaskofu waliokutana na makamu Rais wa nchi Bwana Costantine Chiwenge, ili kujadiliana juu ya mivutano na maandamano yaliyotokea katika wiki za mwisho kwa kusababisha karibia vifo vya watu 12 katika nchi. Kwa mujibu wa melezo ya Padre Chiromba katika muda wa masaa mawili waliweza kuzungumza kwa maelewano na sehemu zote mbili zilionesha utashi wa kushirikana.

Washiriki wa mkutano huo nchini Zimbabwe

Mkutano wa wawakilishi wa Baraza la Maaskofu na serikali ulifanyika tarehe 25 Januari 2019 na kuudhuriwa na Askofu Michael Bhasera, wa Masvingo Rasi mstaafau wa Baraza la Maaskofu Zimbabwe (ZCBC), aliyeongoza uwakilisho kwa niaba ya Rais wa Sasa Askofu Mkuu Robert Ndlovu, wa Jimbo Kuu Katoliki Harare, Askofu Raymond Mupandasekwa wa jimbo Chinhoyi, Askofu Paul Horan, wa jimbo Mutare na askofu Rudolf Nyandoro wa jimbo katoliki Gokwe.  Na kwa upande wa viongozi wa Serikali, walikuwa ni Makamu Rais Bwana Chiwenga, akiambatana na Waziri wa Ulinzi, Oppah Muchinguri na mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha utaratibu wa Usalama, Jenerali Isaac Moyo.

Sababu za ghasia

Sababu za mivutano hii kitaifa ni kuongezeka kwa bei ya mafuta na kusababisha maandamano makuu. Ghasia hizo kati ya waandamanaji na vyombo vya usalama zimepelekea watu elfu moja kuwekwa mbaloni. Rais wa Mnangwagwa ametoa wito wa viongozi wote wa kisisa, kidini na raia ili waweke tofauti zao pembeni  ili kuunganana na kuanza mazungumzo ya kitaifa. Mazungumzo  bado hayajafanyika lakini kuna ulazima wa haraka, na Kanisa liko mstari wa mbele kuona kuwa jambo hili linafanyika anasema Padre Chiromba. Zimbabwe imeshuhudia maandamano jijini Harare, wakati raia wa nchi hiyo wakilalamikia kupanda kwa bei ya mafuta maradufu na Rais Emmerson Mnangagwa anasema ni kwa sababu uchumi umeyumba.

Kanisa limekusanya mashuhuda wa waathirika dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu

Wakati huo huo waathirika wa vurugu mara wanakuja Kanisani na katika mahospitali yao kutafuta msaada na ndiyo kesi ambazo amekwenda nazo  katika serikali kwani ushuhuda huo ni uthibitisho wa dhati kwa kile kinachoendelea kutokea. Padre Chiromba anathibitisha juu ya kesi na mashitaka ya kukiukwaji wa haki za binadamu zilizosababishwa na vikosi vya usalama. Hata hivyo  Padre Chiromba anasema baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yamewaomba watembelee zahanati za Kanisa na huku Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wakikusanya habari kuhusu manyanyaso dhidi ya haki za binadamu na ghasia.

Maaskofu wa Zimbabwe wanashutumu vikali mkono huo mzito wa serikali hivyo ni wazi kuanzisha kwa haraka mazungumzo kati ya sehemu zote mbili ili kuweza kuondokana na kipeo hicho. Katika nchi ya Zimbabwe ukosefu wa ajira ni mkubwa sana kwani ni asilimia 80% za watu hawana ajira. Raia wengi wanamshutumu Rais Emmerson Mnangagwa ambaye alitoa ahadi ya kutumiza wakati wa kufanya kampeni za uchaguzi ili kuboresha uchumi mara baada ya Rais Robert Mugabe ambaye amekuwapo katika madaraka tangu mwaka 1980 na kulazimishwa kujiudhuru urais kunako Novemba 2017.


Maoni


Ingia utoe maoni