Hatimaye baada ya majadiliano ya siku 10 mjini Khartoum nchini Sudan, serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na makundi 14 yenye silaha hatimaye Jumamosi tarehe 2 Januari 2019 wamefikia muafaka wa amani, kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini CAR wa MINUSCA. Kupitia mtandao wake wa Gazeti la la Afrika (https://www.africarivista.it/), MINUSCA imesema makubaliano hayo yamewezekana chini ya mradi wa Afrika kwa ajili ya amani na maridhiano kwa taifa la CAR ulioongozwa na Muungano wa Afrika, AU kama mpatanishi kwa msaada mkuwa wa Umoja wa Mataifa.
Shikamaneni kuunga mkono utekelezaji
Akizungumzia hatua hiyo mkuu wa opereshini za ulinzi wa Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amesema kwenye mtandao wake wa twitter:“Na hebu tushikamane tuunge mkono utekelezaji wa makubaliano haya ya amani”. Naye afisa wa Muungano wa Afrika balozi Smail Chergui ambaye ni Kamishina wa tume ya AU kwa ajili ya amani na usalama amesema: “hii ni siku nzuri sana na muhimu kwa CAR na watu wake wote", wakati huo huo amezitaka pande zote za nchi hiyo kuunga mkono makubaliano hayo na kusema: “yatawezesha watu wa CAR kufuata njia ya maridhiano, umoja na maendeleo.” Pia ameushukuru Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika (AU) kwa mchango wao kufanikisha makubaliano hayo. Baada ya makubaliano hayo yamemtia matumaini Bwana Chergui, kwa kuona pande kinzani sinaingia kwenye majadiliano kwa mara ya kwanza kwa dhamira ya kupata mwafaka. Kamishina huyo amesisitiza ushirikiano ambao ni mfano kwa pande zote. Naye kiongozi wa ujumbe wa serikali ya CAR kwenye mazungumzo hayo mjini Khartoum, Firmin Ngrebad amesema amedhamiria “kufanya kazi na kiongozi wa nchi na serikali yake ili kutekeleza masuala yanayotiliwa mashaka na kaka zetu walioamua kubeba silaha".
Mkutano ulianza tare 25 Januari 2019
Chini ya shinikizo kutoka kwa washiriki wa magharibi, Bangui daima imekuwa inakataa kusamehe wapiganaji wa vita, wengi wao wakiwa chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa au watuhumiwa wa ukiukwaji wa haki za binadamu na mashirika yasiyo ya kiserikali. Mikataba saba ya amani tayari imesainiwa tangu mwanzo wa mgogoro wa Afrika ya Kati, mwishoni mwa 2012, lakini hakuna hata mmoja wao aliyeweza kurejesha utulivu, shirika la habari linakumbusha. Mazungumzo ya amani huko Khartoum ulianza tarehe 25 Januari 2019 na ulikuwa umesitishwa tarehe 30 Januari kutokana na kutokubaliana na habari za wahusika wa kupambana na uharifu na manyanyaso. Makundi ya waasi wenye silaha ya Jamhuri ya Afrika ya Kati walikuwa wameacha mazungumzo ya Khartoum kwa ishara ya maandamano dhidi ya kukataa kwa serikali kukidhi maombi yao, ikiwa na maana ya msamaha kwa ujumla wa wahalifu wa vita na kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa serikali inayoongozwa na waziri mkuu aliyeelekezwa na waasi.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Wakati huo huo, siku chache kabla ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuondoa vikwazo vya silaha zilizowekwa pembeni kwa ajili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mwishoni mwa mwezi Septemba ikiwa mamlaka ya Bangui itaonesha maendeleo ya mchakato wa mageuzi katika uwanja wa usalama na udhibiti wa silaha. Vikwazo vya silaha vilikuwa changamoto hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Afrika ya Kati, Bwana Mathieu Simplice Sarandji, ambaye katika kipimo cha Umoja wa Mataifa alikuwa anaasema hakizuii wanamgambo mahalia wasipate silaha. Mwezi uliopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliongeza mamlaka ya utume wa Minusca kwa mwezi mmoja baada ya kushindwa kupitisha azimio lililowakilishwa na Ufaransa kwa kuomba usuluhishi unaongozwa na Umoja wa Afrika ili kufikia amani ya nchi. Hata hivyo, azimio hili lilikataliwa na Moscow Urusi, ambayo ilikuwa ina kazia juu ya haja ya ushirikiano wa Kiurusi na Sudan.
Hatua zote za hivi karibuni za mazungumzo ya amani kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati zimefanyika kinyume na matashi ya nchi ya Ufaransa na Urusi. Kinacholeta wasiwasi wa Ufaransa ni kutokana na kupenya kwa kasi nchi ya Urusi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, hasa kwenye ardhi ya kijeshi, baada ya Umoja wa Mataifa kuwapa mamlaka Moscow kutoa silaha huko Bangui na kuwapa walimu wa kijeshi mwaka 2017.
Maoni
Ingia utoe maoni