Je kupata ujauzito kwa njia ya kupandikiza mbegu ndiyo njia moja pekee katika kesi ya utasa? Ni njia zipi zilizo za asili? nini maana ya kifo cha hadhi? Hayo na mengine ni maelezo yote ya kisayansi, tafakari za kimaadili, mafundisho ya Kanisa na baadhi ya shuhuda kuhusiana na mantiki hizi na maswali mengine mengi ambayo yamekusanywa kutoka katika ufunguo wa mafundisho ya Maisha ambayo yatapatikana katika app mpya inayowalenga vijana. App hii ya mafundisho ya maisha kwa ajili ya vijana iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, kwa ushirikiano na Chama cha Jérôme Lejeune nchini Ufaransa ambayo inazinduliwa wakati huu wa mchakato wa Siku ya Vijana Panama 2019 na itaendelea kuwapo mara baada ya uzinduzi wake katika mtandao kwa lugha ya kingereza, kiitaliano na kisipanyola kwenye mfumo wa simu zote za Android.
Wazo la app mpya unatokana na kijalida cha maswali kuhusu mambo msingi ya maisha
Maswali na majibu juu ya mada ya msingi ya maisha kwa ajili ya vijana, ambayo yanahusu maendeleo ya kutungwa mimba, ngono na jinsia, magojwa na kifo, utoaji mimba na kutafuta njia mbadala za seli, eutanasia na kupandikiza viungo, yote hayo na mengine yatapatika katika app hiyo kwa ajili ya vijana kujifunza mengi zaidi ya elimu ya viumbe. Hata hivyo wazo la kuunda app hiyo juu ya mada kubwa ya Maisha imetokana na maandalizi ya kujiuliza na kujibu maswali kwa kina , kwa kijalida kidogo kilichokuwa kimeandaliwa na Chama cha Jérôme Lejeune mjini Paris Ufaransa wakati wa tukio la Siku ya vijana huko Rio de Janeiro 2013, kilichokuwa kimeandaliwa kwa luha tofauti na kuwakabidhi vijana mifukoni mwao, kiwasaidie kujisomea wakati wako njiani na kuwagawia wenzao njiani.
Vijana wengi wanatumia simu za mikononi,ni rahisi kuelimishwa kuhusu mambo makuu ya maisha
Akizungumzia kuhusu suala hili la App Bi Gabriella Gambino, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha amesema, miezi ya hivi karibuni wakati wanafanya mandalizi ya siku ya vijana alikutana kwa bahati nzuri na kurasa za kijalida hicho na kuzipitia akitafuta namna ya kuwafanya vijana wawe na umakini juu ya mada msingi wa Elimu ya binadamu, kwa kufikiria tukio la Siku ya vijana Panama. Alifikiria pia kuhusu watoto wake ndani ya familia wenye umri wa ujana kama vijana wengi ambao daima mikononi mwao wameshikilia simu za mikono, wakijaribu kutafuta majibu ya kila swali. Kutokana na fikra hizo ndipo wazo lilitokea la kutengeneza app, ya kutembelea na ili App hiyo iweze kuwasadia kwani wanaweza kupakua kutoka katika simu ya mkono na kujisomea zaidi wakati huo ni zana rahisi ya kutumia anathibitisha. Aidha anasema kwa upande wa vijana ambao wanaweza kukabiliana na mada inayowashirikisha na ambayo kila siku inaingia ndani ya nyumba zote, kwa kufikiria hata kesi ya njia ya ujauzito wa kupandikiza, uchaguzi wa aina ya mtoto, vizuizi vya kuwa na ujauzito, eutanasia, kwa kulinganisha jinsi gani ilivyo ngumu kuelekeza na kujua namna ya kung’amua katika mwanga wa kweli wa wema wa wote amethibtisha.
Changamoto ya kujibidisha katika imani ambayo inakwenda sambamba na maisha ya kimaadili
Siku ya vijana Duniani ni fursa maalum ya uongofu na kukua kwa imani kwa ajili ya vijana wote duniani, lakini pia hata changamoto kubwa zaidi inabaki ile ya kuonesha kwao namna ya kukuza imani na maisha ya kimaadili mambo ambayo ni muhimu kwenda sambamba. Imani inaangazia kwa namna ya ajabu sababu za kibinadamu na uelewa mkubwa wa wema wa kweli. Kwa maana hiyo app katika mtandao inatakuwa zana ya kukuza shauku ya ukweli kwa vijana wengi. Ni mwanzo wa kazi laini ambayo itakuwa ni jukumu kwa watu wazima kuiendeleza na kuitafakari kwa kina katika mafundisho ya katekisimu, shuleni, katika familia au katika jumuiya amethibitisha Bi Gambino katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa,Familia na Maisha.
Maoni
Ingia utoe maoni