Kuongea kichini chini, ukimya kama wa kaburi na hapakuwapo na makofi yoyote, ndivyo viliongoza hali halisi ya makardinali mara baada ya tangazo la Mtakatifu Yohane XXIII kuhusu Mtaguso. Tukio hilo lilijitokeza katika Monasteri ya kibenediktini, kandoni mwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Roma. Aliyekuwa amemsindikiza Mtakatifu Yohane XXIII alikuwa msemaji wake Mkuu Guido Gusso ambaye ni shuhuda wa tukio hili lililotokea tarehe 25 Januari 1959. Guido Gusso aliweza kuingia akiwa kijana kabisa katika Upatriaki wa Venezia kwenye huduma ya Kardinali Angelo Giuseppe Roncalli ( Baadaye atakuwa Papa Yohane XXIII) na ambaye Papa mwenyewe alimwita awe karibu naye baada ya kuchaguliwa kuwa Papa!
Ni mara baada ya miaka 60 sasa, Vatican News imeandaa clip ya video ambayo Gusso anasimulia matukio mbalimbali yanahusu makardinali kukosa neno la kuzungumza, mara baada ya Mtakatifu Yohane XXIII kutoa tangazo la namna hiyo kuhusu Mtaguso. Baadhi walikuwa wakiulizana kichini chini, nini maana ya Mtaguso? Na wengine walionesha hali ya wasiwasi hasa kuhusu gharama za operesheni ya namna hiyo na kufikiria itakuwa ni kukausha sasa vikasha vya Vatican na wengine wakifikiria kwamba ilikuwa ni wiki moja kabla, Mtakatifu Yohane XXIII alikuwa amewaongezea mshahara kwa waajiriwa wote Vatican.
Papa kuwa na mawazo mengi
Gusso anakumbuka hata roho ya Papa, ambayo aliipata kuitambua sana na zaidi kutokana na maandishi yake kwenye kitabu cha kumbu kumbu binafsi kilichotangazwa mara baada ya kifo chake, kimeandikwa vizuri pia kuna ( picha ya tarehe 25 Januari 1959 kwenye Maktaba ya Kipapa ya Yohane XXII , Bergamo Italia). Katika siku hiyo asubuhi Gusso anaonesha kwamba Papa alikuwa na mawazo mengi wakati yuko njiani kuelekea kukutana na Makardinali. Alikuwa mkimya kinyume cha ukawaida wake, kwa maana hakuwa anazungumza. Kabla ya kuondoka lakini kutoka ndani ya vyumba vyake maalum, kinyume chake aliomba kuvaa mavazi mazuri sana na kumwambia msemaji wake mkuu kwamba:"leo itakuwa ni siku ya aina yake kwa sababu ninapaswa kutoa tangazo kuu”.
Safari ya kurudi Vatican na matokeo ya vyombo vya habari
Akiendelea na ufafanuzi anasema wakati anarudi mjini Vatican, papa alisema maneno machache kwamba:“hawakulichukulia vema jambo hili la Mtaguso”. Kwa maana Mtakatifu Yohane XXIII alikuwa ametambua kwa jinsi gani makardinali hawakukubaliana na wazo hili, ameongeza Bwana Gusso. Naye Askofu Mstaafu Luigi Bettazzi wa Ivrea, Italia ambaye ndiye mmojawapo wa mababa wa mtaguso anayeishi bado anathibitisha kuwa, tangazo lisiloeleweka vema kwa makardinali katika Kanisa la Mtakatifu Paulo Roma, lilikuwa halikueleka pia kwa kina katika vyombo vya habari. Mada ya kukabiliana na ushuhuda wa Raniero La Valle Mkurugenzi wa Gazeti la Baraza la Maaskofu Katoliki Italia linaonekana katika Clip ya video kuonesha nyakati za Mtaguso. https://www.vaticannews.va/it/vaticano/news/2019-01/concilio-papa-giovanni-xxxiii-gusso-silenzio-tes...
Mtaguso wa I na Trento ulikuwa bado haujafungwa
Haikuwa bado kufungwa kawaida Mtaguso wa I wa Vatican, ambao ulikuwa umemalizika zaidi ya karne iliyopita wakati wa maingilio ya mapambano ya Mlango wa Pia Rona. Walikuwa bado wana ile taalimungu ya Mtaguso wa Trento na hivyo ni kwa jinsi gani wangeweza kutambua Mtaguso mwingine? Anasema. Kadhalika neno Mtaguso anaeleza, La Vale katika Gazeti la Osservatore Romano kwamba halikuwapo hata katika matangazo ya sura za magazeti ya kwanza. Walikuwa wanazungumza matukio makubwa ya maisha ya Kanisa. Hakuna aliyeweza kuwa makini kuhusu suala hili. Wasingeweza kuwa makini kwa sababu hawakuwa na wazo nini mana ya Mtaguso wa Kanisa la Karne ya XX ambayo ilipaswa kukabiliana na changamoto katika dunia inayobadilika.
Maoni
Ingia utoe maoni