Jumatano. 04 Desemba. 2024
feature-top
Tarehe 27 Januari ya kila mwaka ni Siku ya Ukoma duniani, iliyoanzishwa mwaka 1954

Kila mwaka ifikapo tarehe 27 Januari, inaadhimishwa Siku ya Kimataifa ya ugonjwa wa Ukoma,ambapo ni mwaka wa 66 tangu kuanzishwa kwake kunako mwaka 1954 na Roaul Follereau aliyekuwa mwandishi na mtunzi wa vitabu nchini Ufaransa.Ugonjwa huu bado ni hatari katika mataifa mengi hasa katika nchi nyingi masikini

Tarehe 27 Januari 2019 ni mwaka wa 66 tangu kunzisha Siku ya Ukoma duniani, kunako 1954. Fursa hii inatoa tafakari kubwa juu ya ugonjwa huo na kukusanya fedha, siku iliyoanzishwa tangu mwaka 1954 na Mfuko wa Roaul Follereau aliyekuwa ni mwandishi na mtunzi wa vitabu nchini Ufarasa. Ugonjwa huu bado unameenea katika nchin 153 duniani

Katika kuadhimisha Siku hii, taarifa ni kwamba nchini 153 duniani bado kuna ugonjwa wa ukoma na magonjwa mengine hatarishi, lakini yanayoweza kutibika, japokuwa yanazidi kushambuliwa wanaume, wanawake na watotokatika maeneo yaliyo mengi ya kimasikini duniani. Katika nchini 12 ni asilimia 94 za magonjwa mapya. Chama cha Follereau ambacho utume wake ni ule wa kutibu wagonjwa kimejikita kutoa huduma katika nchi ya ambazo zina kesi kubwa ya ugonjwa wa ukoma duniani kama vile,Mali, Benin,Ivory Coast,GuineaBissau,Niger,Senegal,Congo,Mauritania, Gabon,Madagascar,Tchad,Burkina,Faso,Camerun,Togo,India,Cina,Cambodia na Vietnam.

Bwana Guido Barbera ni mjumbe katika uongozi wa Umoja wa Kitaifa wa Vyama vya Raoul Follereau na Mwenyekiti wa Chama cha Voglio Vivere Onlus cha Italia, moja ya vyama hivi akielezea hali halisi katika mahojiano na Vatican News, amethibitisha juu ya ugojwa wa ukoma unavyozidi kushambulia bado hata kwa miaka hii ya mwisho wanajikita kukabiliana na ugonjwa katika baadhi ya nchi. Na hiyo ni kwa sababu anasisitiza kwamba ukoma umekuwa daima ugnjwa katika nchi nyingi zilizo na umasikini wa kukithiri na zilio pembezoni. Baadhi ya nchi wanazoshughulikia wanaona hali inaizi kuwa mbaya ya maisha. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa duniani (WHO), linathibitisha kuwa, kila mwaka kuna zaidi ya watu 215,000, na 250,000 ni kesi mpya za magonjwa ambayo sehemu kubwa ni kwa ngazi mbaya sana inayosababishwa na kuchelewa kuanza matibabu kwa wale wenye ukoma na ambao wanaishi hasa katika vijiji vilivyotengwa na watu wanajijua kuwa na ugonjwa huo.

Sababu na tiba ya ugonjwa wa ukoma: Sababu msingi za ugonjwa wa ukoma  ni kuendelea kwa umasikini, ukosefu wa huduma ya afya,hupatikanaji wa vyakula, lakini pia hata ujinga, hukumu na kutelekeza kwa upande wa tamaduni nyingi wakiamini kwamba ugonjwa wa ukoma unaambukoa kwa njia ya kupumua na siyo wa kurithi, kinyume chake ni ugonjwa usio ambukiza anathibitisha! Kutibu kwake ugonjwa huo  ni kwa muda mrefu, lakini ni mwafaka. Tume ya madaktari ya Chama cha Follereau imejikita kuwa na ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa kutoa matibabu ambayo yanajikita na madawa ya aina tatu ambayo yanauwezo wa kuuwa bakteria husika. Tiba hiyo inaponya mtu mwenye ugojwa wa ukoma kwa kipindi cha miezi 6 au 12 japokuwa haimrudishi kwa upya  mtu  hali ya kiungo kilichopata ugonjwa huo. Aidha amekumbusha maneno ya mwanzilishi wa siku hiyo Raoul Follereau, yasemayo  “ Nilianzisha Siku ya Ugonjwa wa Ukoma duniani, ili kuhamasisha na kukuza uelewa wa kashifa iliyopo na maoni potofu ya umma kwa ajili ya kusaidia watu masikini ambao wana hali hii na wenye haki ya kupata kille ambacho mtu anahitaji”.

Kutokana na wito wake, anasema kwamba hili  si suala la kutibu mgonjwa tu, bali hata kumpatia hadhi ya binadamu na ambayo ni lazima. Hii ina maana ya kuwa na uhusiano na mgonjwa mara baada ya kupona katika kijiji, japokuwa na shida kidogo. Yote hiyo inatokana na ujinga mbele ya hukumu kuhusiana na mgonjwa wa ukoma, kwani pamoja na kupona kwake ni lazima kutibu hata mitazamo ya kijamii iliyo potofu. Mgonjwa anaporudi katika kjiji chake anabaguliwa, ni katika vijiji ambavyo unakuta hawana ulewa wa ugonjwa huo na kuwasababishia kuwasukuma pembeni. Kwa mujibu wa manono ya mwanzilishi wa siku ya Ukoma duniani anaonesha kuwa bado kuna ukoma mbaya sana wa kijamii unaoitwa ubaguzi wa kijamii na kuwatupa watu pembezoni.

Kanisa na wagonjwa wa ukoma :vituo vya wagonjwa wa ukoma 610  duniani: Kwa mujibu wa takwimu za mwisho za mwaka za Kanisa Katoliki linaendesha duniani vituo vya wagonjwa wa ukoma 610. Barani Afrika 192, Amerika mbili 55, Asia 352, Ulaya 10 na Ocean 1. Mataifa yenye idadi kubwa ya wagonhwa wa Ukoma, Barazni Afrika :Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC (30), Madagascar (25), Kenya (21); Bara la Ameeika ya Kaskazini:Marekani (2); Amerika ya Kati Mexico (9): Antille Haiti (4); Amerika ya Kusini : Brazil (19);Asia: India (243),Indonesia (63), Vietnam (13); Ocean: Papua News Guinea (1); Ulaya: Ujerumani (6), Poland (2). Kanisa la kimisionari lina utamaduni wa muda mrefu la kuwasaidia wagonjwa wa ukoma na mara nyingi waliobaguliwa hata na familia zao. Kanisa limejikita kuwasaidia wao katika kutoa matibabu na kuwasaidia kiroho hasa kwa shughuli ya dhati ya kuwarudishia utu na hadhi yao kwa kuwashirikisha katika jamii. Lakini bado kuna ubaguzi mkubwa sana kwa wagonjwa hawa, kwa kudai kuwa hawaponi magonjwa yao licha ya kusabababisha madhara makubwa ya viungo vyao.

 

Watakatifu waliotoa maisha yao kwa ajili ya wagonjwa wa ukoma: Kuna watatakatifu wengi wa kimisionari ambao wamejitoa maisha yao yote kusaidia wanaoteseka na ugonjwa wa ukoma kama vile Mtakatifu Jozef Daamian De Veuster,anayejulikana sana kama mtume wa wagonjwa wa ukoma wa Molokai, Mtakatifu Marianna Cope aliyejikita kwa miaka 35 huko Molokai akiwa na wafuasi wenzake watatu chini ya shughuli ya Padre Damiani; au Mama Teresa wa Kalcutta na Mwenye heri Jan Beyzym, aliyejikita katika utume wake kati ya wagonjwa wa ukoma huko Madagascar na watumishi wa Mungu Marcello Candia na Raoul Follereau, mwandishi wa vitabu na mwanahabari wa Ufaransa ambaye alianzisha Siku hii tangu 1954 , ambayo leo hii inaadhimishwa kimataifa kwa wagonjwa wote wa ukoma.


Maoni


Ingia utoe maoni